Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka, ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali
wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara wa Halmashauri
mkoani hapa jumla ya vitambulisho 25,000, vitakavyotolewa kwa
wajasiriamali wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.
Akikabidhi
vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia wajasiriamali wadogo
kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu na kuwafanya kunufaika
na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa vitachangia pia kuwaibua
wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.
Ameongeza
kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa
na Mhe. Rais, huku akiwaonya na kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa
wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia
vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa njia ya udanganyifu.
“Niwatahadharishe
wafanyabiashara wasije wakatumia nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali
wadogo, kufanya udanganyifu wowote wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo
kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo; huu udanganyifu hatutaupa nafasi na
sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha kila mtu anachofanya, mahali anapokaa,
historia yake ya biashara”
“Ofisi
za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha maafisa Biashara kwenda
vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini walengwa wa vitambulisho hivi
ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo
fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho hicho,kwa hiyo kuna kadi
zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali walipo walengwa”
alifafanua Mtaka.
Baadhi ya wakuu wa wilaya wakizungumza mara baada
ya kupokea vitambulisho hivyo wamesema watahakikisha vinawafikia walengwa
waliokusudiwa na hakutakuwepo na udanganyifu wowote katika zoezi la ugawaji wa
vitambulisho hivyo.
“Niwahakikishie wajasiriamali wadogo wote kuwa
watapata vitambulisho kama Mhe Rais alivyoelekeza na nitoe wito kwao kuja
kuchukua vitambulisho hivi ili asiwepo mtu yeyote wa kuwabugudhi na wafanye
kazi zao kwa uhuru” Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
“ Niwatoe hofu wajasiriamali wote wadogo kuwa kila
aliye na sifa ya kupata kitambulisho hiki atapata na kwa wale wanaodhani
watatumia vitambulisho hivi kukwepa kodi nichukue nafasi hii kutoa onyo kuwa
hatutavumilia udanganyifu wa aina yoyote” Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe. Tano
Mwera.
Baadhi ya wajasiriamali Wadogo Mkoa Simiyu
wameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe
Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vitawaondolea adha
mbalimbali walizokuwa wakizipata ikiwepo ya kuogopa kufanya biashar zao
kutokana na kutotambuliwa rasmi.
“ Tanamshukuru sana Rais ametupa ujasiri wa kufanya
biashara zetu kwa uhuru maana kuna watu walikuwa wanaogopa kufanya biashara kwa
sababu ya kuogopa kodi, kupitia vitambulisho hivi tutafanya biashara kwa
uaminifu, uhuru na ujasiri na katika wilaya yetu ya Bariadi, Tanzania ya
Viwanda hasa vile vidogo itawezekana” alisema Bahati Kaitila mjasiriamali
mdogo kutoka Bariadi.
“ Nimelipokea vizuri suala la kupewa vitambulisho
kwa sababu vitatusaidia sisi wajasiriamali wadogo kupata ujasiri zaidi wa
kufanya kazi zetu, tunaweza kuanza na kitu kidogo lakini baadaye tukafanya
makubwa” alisema Grace Mukali mjasiriamali mdogo kutoka wilaya ya
Bariadi.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment