METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 11, 2018

MHE BITEKO AITAKA MMC KUWALIPA WANANCHI FIDIA YAO ILI WAWEZE KUENDELEA NA UCHIMBAJI


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katika) akikagua mgodi wa MMC wa dhahabu uliopo Wilayani Mvomero mkoani Morogoro jana tarehe 9 Desemba, 2018.  



Mwakilishi wa Mgodi wa MMC upande wa uzalishaji (wa kwanza kulia), akimwelekeza jambo Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) wakati alipokuwa akikagua mgodi huo alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa migodi ya dhahabu Mkoani Morogoro hapo jana tarehe 9 Decemba, 2018.

Wananchi wa Vijiji vya Mtukule na Mangae wakimsikiliza Naibu Waziri wa madini, Doto Biteko jana tarehe 9 Disemba, 2018 Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.


Muonekano wa Mgodi wa MMC uliopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

v Wachimbaji wadogo nchini kote mnapoingia mikataba lazima Serikali itabue mikataba hiyo.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ameutaka Mgodi wa MMC kulipa fidia kwa wananchi wa vijiji vya Mtukule na Mangae ambao walipisha mgodi huo lakini hawakuwahi kulipwa fidia yao.

Naibu Waziri Madini Doto Biteko ametoa maagizo hayo jana tarehe 9 Desemba, 2018 alipotembelea Mgodi wa MMC lengo likiwa ni kukagua shughuli zilizokuwa zikiendelea za uchimbaji pamoja na kuwa waliagizwa kusimama kufanya shughuli hizo hadi watakapo lipa fidia kwa wananchi hao wanaodai haki yao.

Biteko ameeleza kuwa tangu Mgodi huu kuanza umekuwa ukiendelea na shughuli zake za uchimbaji lakini wananchi waliouzingira mgodi huu hawajelipwa haki yao, lepeni fidia kwanza alafu kama uwekezaji wenu ni halali mtaendelea.

“MMC hakikishani kuwa wananchi wote wanalipwa haki yao na sio laki tano niliyoambiwa kuwa wamelipwa,” alisema Biteko.

Aidha, Biteko amemwagiza Mkuu wa Wilaya wa Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally kuhakikishe kuwa, wananchi wote wanachambuliwa ili kujua mwenye haki ya kulipwa na kama ardhi ni ya kijiji ijulikane ni kiasi gani ili kila mmoja wao alipwe haki yao, ili kama uwekezaji ni wa haki wananchi wapishe uwekezaji huo.

Biteko aliendelea kueleza kuwa maendelea hayawezi kupatikana kama mgodi na wananchi hawako vizuri, lazima wawekezaji wapitia hatua mbalimbali kama vile ya kujitambulisha kwa Serikali ya Kijiji hadi ya Wilaya.

“Na ili Mgodi huu uwe na adhabu lazima shughuli zake za uchimbaji zisimame hadi hapo watakapokuwa wamelipa wananchi fidia yao, alisema Naibu Madini Biteko.

Akizungumza katika hadha hiyo, Biteko alisema kuwa wananchi pia wamepeta adha ya barabara, na wamelazimishwa kupita barabara nyingine ambayo hairidhishi.

Nakwagiza Mkuu wa wilaya na hili pia ulifanyie kazi kwa kushirikiana na Mkuu wa TARURA mkoa ili wananchi hawa wapate haki yao.

“Tunataka tuondoe ubabaishaji na uongouongo kwenye Sekta ya Madini,” alisema Biteko.

Pia, Naibu Waziri wa Madini Biteko ametoa wito kwa Watanzania wote hasa Wachimbaji wadogo kuhakikishe kuwa, kila wanapoingia mikataba na Wawekezaji wageni lazima Serikali itambue mikataba hiyo.

Biteko aliongeza kuwa, lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa watanzania hawanyonywi na vile vile wawekezaji hawaingii mikataba ambayo sio sahihi alafu baadaye wanalaumu serikali ya Tanzania kuwa inanyanyasa wawekazaji.

Aliongeza kuwa sisi Watanzania tusiwaingize wawekezaji mkenge alafu nchi ya Tanzania inaonekane kuwa inawanyanyasa wawekezaji, futeni sharia zilizopo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally alihaidi kuwa atayafanyia kazi maagizo haya na atasimamia kuhakikisha kuwa kila mwananchi analipwa haki yake.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com