Katibu Mkuu
Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akimkaribisha Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga kufungua Kikao kazi
Wakuu wa Taasisi za Haki Jinai kuhusu Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai
kinachofanyika katika Hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma
Baadhi ya
washiriki wa kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa Kikao Kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai.
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga akisoma hotuba yake
kabla ya kufungua kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki jinai.
………………..
Na.Alex Mathias,Dodoma
SERIKALI imesema ipo katika mchakato
kufanya maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai nchini ili kuendana na
kasi kubwa ya mabadiliko duniani yanayotokea katika nyanja mbalimbali.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na
Waziri wa katiba na sheria Balozi Augustine Mahiga, wakati alipokuwa
akifungua mkutano wa maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai
uliowajumuisha wataalam kutoka wizara na taasisi mbalimbali nchini.
Amesema kuwa wao kama serikali wanao
wajibu wa kufanya maboresho mbalimbali ya sekta hiyo ya haki jinai ili
kuendana na wakati ulipo sasa.
“Ndugu washriki nchi yetu na dunia kwa
ujumla zimeshudia kasi kubwa ya mabadiliko yatokanayo katika nyanja zote
za maisha, kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kiteknolojia hali
ambayo imesababisha kuwepo kwa mbinu mpya za uharifu ambazo
ushughulikiaji wake unahitaji kuendana na mabadiloko hayo”amesema.
Aidha amebainisha kuwa kutokana na kuwepo
kwa hali hiyo Wizara na wadau waliona umuhimu wa kufanya majadilinao ya
pamoja kwa lengo la kuboresha sekta ndogo ya haki jinai.
Amebainisha kuwa maboresho yanayotarajiwa
yatajumuisha maeneo yote yenye changamoto yakiwemo ya kisera, kisheria
na kiorganizesheni ili kuufanya mfumo huo kuweza kuakisi changamoto za
maendeleo za kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Pia amesema sekta hiyo ndogo ya haki
jinai bado inakabiliwa na changamoto kama vile majengo ya mahakama
ambayo yamejengwa toka wakati wa mkoloni.
Ameongeza kuwa maboresho hayo yatasaidia katika kukidhi ongezeko la watu ambalo limekuwepo havi sasa nchini.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, amesema maboresho ya mfumo wa haki
jinai yatasaidia kulifanya taifa kuwa na jamii ya watu waliostaarabika
na kuheshimu utawala wa sheria pamoja na kutunza amani na utajiri wa
rasilimali.
“Marekebisho hayo yanasaidia katika
kutengeneza taifa ambalo limestaarabika na kuwa na jamii ambayo
inafuata na kuheshimu taratibu za nchi yao” amesema.
Amebainisha mfumo wa haki jinai unafanya
kazi kwa mfumo wa mnyororo wa taasisi katika kuhakikisha wananchi
wanapata haki na kupambana na uharifu wa aina yeyote ukiwemo ule wa
kimataifa.
0 comments:
Post a Comment