Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya kilimo)
Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akielezea muundo na majukumu ya wizara ya kilimo kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa kilimo Mhe Japhet Hasunga ameshangazwa na miradi mingi iliyopo katika wizara
ya kilimo huku ikiwa na uchache wa manufaa.
Amesema
kuwa wataalamu mbalimbali waliopo katika wizara hiyo wanapaswa kutekeleza
wajibu wao kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza
tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.
Waziri
Hasunga ameyasema hayo tarehe 21 Novemba 2018 wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi
wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na
Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi.
Katika
kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) kikiwa na dhumuni la kufahamiana ambapo washiriki wamepata fursa
ya kueleza namna ambavyo kilimo kinaweza kuimarika na kuwanufaisha wakulima
nchini.
“Lazima
tuendelee maana rasilimali watu zipo, wasomi wazuri wapo na tafiti zipo hivyo
hatuna sababu ya kushindwa kufanikiwa kwenye sekta ya kilimo” Alikaririwa Mhe
Hasunga na kuongeza kuwa
“Kuna
watu wamepewa rasilimali kubwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini ufanisi wao
na tija katika utendaji ni mdogo sana jambo hili halikubaliki lazima tubadilike”
Kwa
upande wake Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akichangia katika kikao
hicho alisema kuwa tarehe 4 Juni 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua programU ya kuendeleza sekta ya kilimo
awamu ya pili (ASDP II) huku kukiwa bado kuna mapungufu makubwa kwenye ASDP
awamu ya kwanza.
Alisema
kuwa katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ASDP kulitakiwa kujengwa vituo
vya kata vya elimu kwa wakulima vya nadharia na vitendo kwani Vilivyojengwa ni vichache
huku vikiwa vimebadilishiwa matumizi tofauti na mtazamo uliotakiwa awali.
Pia
alisisitiza kusimamiwa ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wizara ya kilimo ili
kukabiliana na soko la mazao katika soko la Dunia.
Vilevile
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa katika
kuimarisha kilimo nchini Tume ya Maendeleo ya ushirika inapaswa kusimamiwa kwa
weledi mkubwa kwani mafanikio ya mkulima yapo katika muungano wa pamoja ili
kuwa na weledi katika kupanga bei ya mazao wanayolima.
Sambamba
na hayo Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa serikali inajidhatiti katika kuimarisha
masoko ya wakulima nchini kwani wakulima wamekuwa wakizalisha mazao mengi
lakini changamoto inasalia kukosekana kwa masoko.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment