Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali na Sekta binafsi
katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani
Simiyu ambayo imefanyika mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha
Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa
akifafanua jambo katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali
na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa
Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano
katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa viongozi wa
Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa
Serikali na sekta binafsi wakifuatilia Warsha ya Utetezi na majadiliano
katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa viongozi wa
Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mjini Bariadi
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Shule ya biashara, Khalidi Swabiri (mwezeshaji) akitoa mada katika
Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu,
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Bariadi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato(TRA) Mkoa wa
Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa akifafanua jambo katika Warsha ya Utetezi
na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa
viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika
mwishoni mwa wiki mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson
Kilangi akichangia hoja katika Warsha ya Utetezi na majadiliano katika
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali
na sekta binafsi mkoani Simiyu iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini
Bariadi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Shule ya biashara, Khalidi Swabiri (mwezeshaji) akitoa mada katika
Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu,
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Bariadi.
………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amewataka viongozi wa Serikali mkoani Simiyu kuisaidia na kuilea
Sekta Binafsi ili iendelee kukua na wahakikishe kuwa maamuzi wanayofanya
hayawi vikwazo katika mazingira ya biashara na uwekezaji.
Mtaka ameyasema hayo wakati akifungua
Warsha ya Utetezi na majadiliano katika kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji kwa viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani Simiyu
ambayo imefanyika mjini Bariadi.
Amesema viongozi wa Serikali mkoani humo
wanapofanya maamuzi katika biashara za watu ni lazima wawe na nia ya
dhati ya kuona sekta binafsi inakuwa, ili maamuzi ya viongozi hao yasiwe
vikwazo kwa ukuaji wa Sekta binafsi na mazingira ya biashara na
uwekezaji.
“Sekta binafsi ni lazima ilelewe anaeilea
ni Serikali, Sekta binafsi ni lazima ilindwe anayeilinda ni
Serikali,Sekta binafsi ni lazima isimamiwe anayeisimamia ni Serikali na
Serikali inaisimamia kwa maana ya kuilea ili ifanye vizuri” alisema
Mtaka.
Aidha, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya
mkoani Simiyu kuendeleza utaratibu wa kukutana na wafanyabishara ili
kupata nafasi ya kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji na
namna ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, huku akisisitiza
pia kuendelea kufanyika kwa mabaraza ya biashara ya wilaya.
Katibu wa Chama cha Wafanyabiashara,
Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA) Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya
amesema ili kuboresha mazingira ya biashara Serikali inapaswa kuendelea
kuvutia wawekezaji na kusimamia sheria, sera na kanuni zisipindishwe,
huku akiupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuandaa mwongozo wa uwekezaji.
Katika hatua nyingine Meneja wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Mkumbwa ametoa
wito kwa wafanyabiashara kuwa wazalendo, kutoa risiti ipasavyo, kufuata
sheria za kodi na akaahidi kuwapa ushirikiano wafanyabiashara kila
wanapohitaji.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Shule ya biashara, Khalidi Swabiri ambaye alikuwa mwezeshaji wa warsha
hii amesema ni vema mabaraza ya biashara ya wilaya yakafanyika ili
wafanyabiashara wapate muda wa kukutana na viongozi wa Serikali, sekta
binafsi kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
katika mazingira ya biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Chama cha
Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA), Dkt. Meshack Kulwa
amesema pamoja na kuomba mabaraza ya biashara ya wilaya yafanye kazi,
ameomba TCCIA mkoani Simiyu itafute viongozi watakaofanya kazi kwa
kujituma ili TCCIA Simiyu iweze kuwa imara
0 comments:
Post a Comment