Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Novemba 20,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wanawake waliojitokeza kushiriki
katika ujenzi wa Shule ya Msingi katika kijiji cha
Kilimahewa wilayani Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipowasili kwenye eneo la ujenzi wa shule hiyo kukagua ujenzi na
kushiriki katika ujenzi huo, Novemba 20, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwaamewapongeza wakazi wa kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa kwa kujenga
shule ya msingi kwenye kijiji cha Kilimahewa.
“Uamuzi wa kujenga shule ya
msingi ni sahihi kwa kuwa huwapunguzia watoto kutembea umbali mrefu na pia
utarahisisha mazingira ya kusomea kwa watoto wetu.”
Waziri Mkuu ametoa pongezi
hizo leo (Jumanne, Novemba 20, 2018) alipotembelea eneo la ujenzi wa shule ya
msingi Lugalo na kuwataka waendelee na moyo huo.
Amesema Serikali ya Awamu
ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtoto aliyefikia
umri wa kwenda shule aanzishwe shule na asome.
Kadhalika, Waziri Mkuu
ametaka wananchi hao waweke pembeni itikadi zao za kisiasa na badala yake
washirikiane kujenga miradi ya maendeleo kwenye eneo lao.
Nae, Mtendaji wa Kijiji cha Kilimahewa, Majuto Ungulu
amesema ujenzi wa shule hiyo uliibuliwa na wakazi wa kijiji hicho, ambacho
hakina shule ya msingi.
Majuto amesema watoto wa
kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa kilomita mbili hadi shule la
msingi Ruangwa, hivyo ujenzi huo utawawezesha kusoma karibu.
Amesema kwa sasa wameanzia
na ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa, matundu 18 ya vyoo na ofisi mbili za
walimu ambapo jumla yake ni sh. milioni 399.8.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea kituo cha afya cha
Mbekenyera na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwataka
wananchi wakitunze.
Amesema kwa sasa wananchi
hao hawana sababu ya kulipa nauli kwenda Ruangwa kufuata huduma za vipimo na
matibabu katika hospitali ya wilaya.
Ametaja baadhi ya huduma
zinazopatikana kwa sasa kwenye kituo cha Afya Mbekenyera ambazo awali
hazikuwepo ni upasuaji, maabara, mama na mtoto.
Mapema, Waziri Mkuu
alikagua eneo la ujenzi wa kituo cha Polisi Ruangwa, alitembelea mradi wa
ujenzi wa Mahakama ya wilaya na kukagua ujenzi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.
0 comments:
Post a Comment