KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AONGOZA OPARESHENI YA UKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI JIJINI DODOMA
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Injinia Joseph Malongo akiongea wakati wa uzinduzi wa operesheni ya
zuio la mifuko la mifuko ya plastiki ilyofanyika jijini Dodoma ikiwa ni
agizo la Serikali kuwa ifikapo tarehe 1 juni hakuna tena kutumia mifuko
ya plastiki
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Injinia Joseph Malongo akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha
kuzuia mifuko ya plastiki jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa operesheni
ya kukagua mifuko ya plastiki jijini humo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Injinia Joseph Malongo akiwa pamoja na Katibu Tawala mkoa wa Dodoma
wakati wa ukaguzi wa mifuko ya plastiki kwenye maduka na masoko jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,
Injinia Joseph Malongo akinunua kikapu ikiwa ni kuhamasisha viongozi
kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki jijini Dodoma
Sehemu ya Wakazi wa jiji la Dodoma waliohudhuria katika uzinduzi wa operesheni ya ukaguzi wa mifukoya plastiki jijini Dodoma.
…………………..
Wito umetolewa kwa Wakazi wa Dodoma na
Wilaya zake kuacha kabisa kautumia mifuko ya plastiki na kuanza mara
moja matumizi ya mifuko mbadala ikiwa ni kutii agizo la Serikali la
kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo wakati wa uzinduzi wa operesheni
ya kukagua mifuko ya plastiki katika jiji la Dodoma ambapo ni kutii
agizo la Serikali la ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia
juni 1.
Akiongea katika oparesheni hiyo amesema
kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo Wasimamizi wakubwa wa mazingira
Nchini, hivyo amefurahi kuona elimu juu ya katazo la mifuko ya plastiki
kwa jiji la Dodoma imefika kwa Wananchi kwa sababu ambao wamekutwa na
mifuko ya plastiki ni wachache sana kulinganisha na Wananchi wanaotumia
mifuko mbadala kwa siku ya leo. ‘Elimu imefika kwani kila Mwananchi
namuona kabeba mfuko mbadala, vikapu n.k” alisema Injinia Malongo
Naye Mkuu wa Wilaya wa jiji la Dodoma Mh.
Protabas Katambi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na anawaagiza
Wananchi na Wafanyabiashra wa jiji laDodoma kutii agizo la Serikali na
kuachana kabisaa na matumizi ya mifuko ya plastiki. ‘Mwananchi
atakayekutwa na mfuko wa plastiki hatua kali za kisheria zitachukuliwa
juu yake, hili suala syo mchezo mchezo nia agizo la Serikali” alisema
Katambi
Operesheni hiyo ya kukagua mifuko ya
plastiki imekuja baada ya Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kutoa agizo bungeni kuwa ifikapo juni 1
hakuna Mwananachi atakayeruhusiwa kutumia mifuko ya plastiki Nchini
Tanzania.
No comments:
Post a Comment