Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mfanyabiashara, Justina Damas, Soko la Jioni la Mwanga mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, juu ya Uboreshaji wa chanja za kuanika dagaa katika mwalo wa Soko la samaki la Kibirizi wakati akikagua shughuli za Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,
Na. OWM, Kigoma.
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza
la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na
Uwekezaji unaotekelezwa katika mkoa wa Kigoma na Dodoma, umefanikiwa kuboresha
Mazingira ya Biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa
kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 16 hadi kufikia Desemba 2018.
Mradi huo ambao utekelezaji wake
unajikita katika Uwekezaji na Biashara katika Halmashauri kupitia mfuko wa
(SIFF), Kuimarisha minyororo ya thamani pamoja na kuimarisha majadiliano kati
ya Serikali na Sekta Binafsi, tayari umefanikiwa kuboresha Mazingira ya
Biashara kwa Wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma.
Akiongea katika ziara yake mkoani
Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la
Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana
na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la
Biashara kwa kushirikiana na Mradi huo wameweza Kuwawezesha wananchi kiuchumi
kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo midogo inayochochea ongezeko la ajira na
kipato.
“Nimetembelea Mwalo
na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi Mradi huu
ulivyoboresha miundo mbinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza
upotevu wa mazao ya samaki na dagaa. Niyaombe Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na
Wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili
kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika” Alisisitiza Mhagama.
Mhagama
alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza
kupunguza vikwazo na kero kwa wafanyabiashara lakini pia Kuimarishwa kwa
mahusiano kati ya Serikalii na Sekta Binafsi na kuongezeka
kwa ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Mipango ya
Serikali.
Awali akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa Mradi huo, Mratibu wa Mradi (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya
Umma na Binafsi), Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha
kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari
umeandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya
Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na
yenye ufanisi ambapo Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana.
Katika
ziara hiyo, Waziri Mhagama, pamoja na kutembelea mwalo wa soko la Samaki la
Kibirizi waziri alitembelea Kituo cha Biashara (One Stop Business Centre –
Kigoma), Soko la Jioni la Mwanga, na Mradi wa Kuwezesha Vijana Kushiriki katika
Kilimo Biashara na Mnada wa Mifugo Buhigwe.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment