Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (Kulia) akikabidhi vitambulisho vya wajasiliamali kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukw Mh. Joachim Wangabo amewatahadharisha wafanyabiashara watakaogushi
taarifa kwa nia ya kupatiwa vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dk.John Pombe
Magufuli kwaajili ya wajasiliamali wadogowadogo kote nchini walio na mitaji
isiyozidi shilingi milioni nne.
Amesema
kuwa jukumu lake ni kuvikabidhi kwa wakuu wake wa wilaya ili nao kuvifikisha
kwa wakurugenzi na hatimae kuwafikia walengwa wa vitambulisho hivyo na kuongeza
kuwa wajasiliamali waondoe shaka juu ya idadi ya vitambulisho hivyo kwani
vikiisha vitaagizwa vingine na hakuna atakaekosa.
“20,000/=
kwa kila kitambulisho, lakini kwa mtu yeyote yule ambae atakuwa “amefoji” ambae
atapewa kitambulisho bila ya kustahili atanyang’anywa kitambulisho hicho na
20,000/= hazitarudi, kwahiyo nitoe angalizo kwa hawa wajasiliamali wadogo
wadogo wazingatie hizo taratibu ambazo zimewekwa,” Alisisitiza.
Ameyasema
hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vitambulisho hivyo 25,000, kwa wakuu wa
Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi zenye halmashauri nne, hivyo kila
halmashauri kupatiwa vitambulisho 6,250.
Wakati
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, katibu Tawala wa Mkoa huo Bernard Makali
alitahadharisha kuwa vitambulisho hivyo vina alama maalum ambayo haionekani kwa
macho na kuonya kuwa wananchi wasijidanganye wala kuthubutu kugushi popote
walipo.
Awali
akisoma masharti ya kupatiwa kitambulisho hicho Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA)
mkoa wa Rukwa Fredrick Kanyiriri alisema kuwa miongoni mwa mashari ya
mjasiliamali atakayekabidhiwa kitambulisho hicho ni pamoja na mjasiliamali huyo
kujaza fomu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kujipambanua kwamba mauzo yake
hayafiki shilingi milioni nne kwa mwaka na kulipa shilingi 20,000/= ambayo
itaingia katika akaunti kodi za ndani.
Pia
alifafanua “Sharti la pili ni lazima mjasiriamali huyo lazima awe hajasajiliwa
TRA kwa maana ya hana namba ya utambulisho (TIN) isipokuwa tu kwa wale
waliopata namba ya utambulisho huko mwanzoni kwasababau mchakato huu ulianzia
TRA wa kuwatambua wajasiliamali hawa lakini lakini baada ya kukwama Mh. Rais
aliamua auchukue na kuuweka katika utaratibu mwingine lakini kuna wenye TIN.”
0 comments:
Post a Comment