Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza Jasi (Gypsum
Board) cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa lengo la
kukagua mazingira ya wawekezaji wa kiwanda hicho kwa nia ya kuendelea
kuboresha mazingira yao ziara ilifanyika Juni 28, 2019.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akihutubia washiriki wa mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda cha KNAUF ili
kuzungumza nao masuala ya uboreshaji wa mazingira ya wawekezaji nchini
wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.Meneja
wa Mradi kutoka kiwanda cha KNAUF Bw. Norbert Wagner akimuonesha
michoro ya ramani ya kiwanda hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea na kukagua mazingira yao
Juni 28, 2019.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
akiangalia moja ya malighali zinazotumika katika kiwanda cha KNAUF
(Metal Profile) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda
hicho na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo.Meneja
Uzalishaji Bw. Nurdin Bofu akimuonesha jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki wakati wa ziara yake
katika kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipata
maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara
kuhusu namna wanavyopakia unga maalumu wa kutengeneza jasi wakati wa
ujenzi wakati wa ziara yake.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
akiangalai moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda kinachotengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika ziara ya kukagua kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Mkuranga Pwani.Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akihutubia washiriki wa mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda cha KNAUF ili
kuzungumza nao masuala ya uboreshaji wa mazingira ya wawekezaji nchini.
Meneja Fedha wa kiwanda cha KNAUF
akiwasilisha hotuba kuhusu kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki kiwandani
hapo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………….
NA.MWANDISHI WETU – OWM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuka ameutaka
uongozi wa kiwanda kinachotengeneza bidhaa za cha za jasi (Gypsumboard) cha KNAUF kuendelea kushirikiana na jamii inayowazunguka katika kujiletee maendeleo.
Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa
wiki hii alipotembelea kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili kukagua shughuli za uzalishaji
zinazoendela pamoja na kusikiliza changamoto za wawekezaji hao na kuweza
kujadili masuala ya kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na
uwekezaji nchini.
Waziri Kairuki aliwataka kuona umuhimu wa
kuchangia katika shughuli za kimaendeleo katika maeneo yanayozunguka
kiwanda hicho hususan katika uboreshaji wa miundombinu na utoaji wa
misaada itakayofikia jamii kwa sehemu kubwa na si mtu mmoja mmoja ili
kuleta maendeleo katika eneo kubwa na kuondoa tofauti kubwa za
kimaendeleo zisizoendana na maendeleo ya maeneo kiwanda hicho.
“Ni muhimu sana, na ni busara kuona ni
kwa namna gani mnashirikiana na wananchi wanaozunguka eneo hili katika
kuleta maendeleo ili kuhakikisha mnakubalika , na kuleta maendeleo ya
eneo husika na kuondoa tofauti za kimaendeleo kati ya ustawi wa kiwanda
na jamii inayowazunguka”alieleza Waziri Kairuki
Waziri aliutaka uongozi huo kushiriki
kimalilifu katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia kuboresha
miundombinu inayozunguka mazingira ya kiwanda ili kuendelea kushiriki
kwa vitendo na kuunga mkono jitihada za kuendelea eneo hilo.
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jumaa Abeld aliomba uongozi wa
kiwanda kuona namna ya kuchangia katika maendeleo ya eneo lao kwa
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa sita katika shule ya msingi ya
Kitangwi pamoja na madarasa manne katika shule ya msingi ya Kisemvule
zilizopo Wialya ya Mkuranga katika mkoa huo.
“Ombi letu ni kuona namna kiwanda hiki
kinavyoweza kuchangia katika maendeleo kwa kutujengea vyumba sita vya
madarasa katika shule zinazotuzunguka ili kusaidia uhaba uliopo na
kusaidi watoto wetu kujifunza katika mazingira mazuri,”alisema Jumaa.
Aidha Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi.
Zainab Mwasara aliahidi ifikapo Julai 05 mwaka huu uongozi wa kiwanda
utatoa taarifa za utekelezaji wa maombi hayo ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa 6.
“Tunaahidi kukutana kama uongozi wa
kiwanda ili kujadili na kutekeleza masuala ya msingi ikiwemo hili la
ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuendelea kuleta tija kwa uwepo wa
kiwanda katika eneo hili,”alisema Mwasara.
Naye, Meneja Fedha wa kiwanda hicho Bi.
Wema Mboga alishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya
wawekezaji nchini na kumpongeza ziara ya Waziri katika kutatua na
kuahidi kufanyia kazi masuala yaliyoelezwa kuwa ni changamoto kiwandani
hapo ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika,
kutokamili kwa leseni za uchimbaji kwa wakati, tozo kubwa za malighafi
na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kiwandani hapo.
AWALI
Kiwanda cha KNAUF kilianzishwa mwezi Novemba mwaka 2015 kwa lengo la kuzalisha bidhaa za jasi (Gypsum board), gundi za jasi, pamoja na chuma za jasi (metal profile) kufanya
kazi na usambazaj.Kiwanda kinafanya kazi katika nchi zaidi ya 80 ambapo
katika nchi za kusini mwa Janga la Sahara, Tanzania ni nchi pekee
ambayo ina uwekezaji huo kutokana na sababu za mazingira mazuri ya
kibiashara na uwekezaji pamoja na sababu za kijiografia.Kampuni imeajiri
wazawa 150 katika Nyanja zote kwa kulenga ifikapo 2020 kiwanda kiweze
kuendeshwa na wazawa pasipo kutegemea wataalam kutoka nje.
0 comments:
Post a Comment