Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika leo tarehe 9 Mei, 2019 Mtumba Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo Ndg Obey Assery akitoa maelezo ya awali mbele ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika leo tarehe 9 Mei, 2019 Mtumba Jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Menejimenti ya Wizara ya Kilimo wakifatilia maelekezo ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika leo tarehe 9 Mei, 2019 Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifatilia kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara ya Kilimo kilichofanyika leo tarehe 9 Mei, 2019 Mtumba Jijini Dodoma.
Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 9 Mei, 2019 ameiagiza
Timu ya wataalamu wa wizara ya Kilimo ambao wametuama kuandaa rasimu ya sheria ya
kilimo na kufikia mwezi Julai 2019 iwe imekamilika.
Alisema kuwa ipo
haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto
zinazomkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla hivyo ili kufikia malengo hayo
ni lazima kuwa na ukomo wa ukamilishaji wa mpango kazi huo.
Waziri Hasunga
ameyasema hayo leo tarehe 9 Mei 2019 wakati wa kikao na Menejimenti ya Wizara
ya Kilimo, kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent
Bashungwa, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
“Kuna kila
sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo
na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia
inahitaji kuboreshwa ili iweze kuendana na mabadiliko mbalimbali ya kisera na
wakati, ambapo lazima tuwe na rasimu yake kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Mei”
amesema
Mhe. Hasunga
ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali,
ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba
kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.
Mazao yaliyo
katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho,
Pareto, Mkonge, Sukari na Tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara, mazao ambayo
hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa
Taifa.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) alisema kikao hicho ni
cha kipekee kwakuwa kitapelekea kuimarisha mkakati wa pamoja wa Wizara ya
kilimo kuwa na uelekeo katika utatuzi wa kero za wakulima kisheria.
Aidha,
alipendekeza kuwa ni vyema sekta ya ushirika ikatajwa kwa umuhimu wake kwenye
sera ya kilimo sambamba na Zana ndogo za Kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment