Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Julius Kadawi akisisitiza kuhusu nafasi zilizotolewa kwa vijana wanaopenda kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea kwa mwaka 2020, hayo yemejiri leo Agosti 20, 2020 Makao Makuu ya Jeshi hilo Chamwino mkoani Dodoma.
Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) latangaza nafasi
za kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo kwa kujitolea mwaka 2020.
Hayo
yamesemwa leo Agosti 20 Makao Makuu ya Jeshi hilo, Chamwino mkoani Dodoma na
Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi hilo, Kanali Julius Kadawi ambapo amesema kuwa,
Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Charles Mbuge anawatangazia vijana wote wa
Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo hayo ili waweze
kujengewa stadi za kuweza kujiajiri na kuwa wazalendo.
“Jeshi
la Kujenga Taifa linapenda kuwaarifu vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi
ajira kwa vijana, pia halihusiki kuwatafutia vijana ajira katika asasi, vyombo
vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya
Kiserikali”, alisisitiza Kanali Kadawi.
Aliongeza
kuwa uratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo,
unaratibiwa na Ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambako mwombaji anaishi.
Akifafanua
amesema kuwa Jeshi hilo linatoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri
wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na JKT.
“Kutokana
na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID- 19), tahadhari za kuzuia maambukizi
ya ugonjwa huo kama zilivyoelekezwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya
zitazingatiwa kwa kipindi chote vijana watakapokuwa katika mafunzo,” alisisitiza
Kanali Kadawi
Aidha,
alibainisha kuwa Meja Jenerali Charles
Mbuge anawaalika vijana wote watakaopata fursa hiyo kwenda kujifunza uzalendo,
ukakamavu, stadi za kazi, stadi za maisha na pia kuwa tayari kulilinda na kulitumikia Taifa.
Baadhi
ya sifa za vijna wanaotakiwa ni pamoja na; kuwa raia wa Tanzania, awe na afya
njema, mwenye nidhamu na tabia nzuri na hajawahi kupatikana na hatia Mahakamani
na hajawahi kufungwa, asiwe ametumikia Jeshi la Magereza, Polisi, KMKM, Chuo
cha Mafunzo, wala kuajiriwa na idara nyingine Serikalini.
Kigezo
kingine asiwe amepitia JKT katika operesheni za nyuma, asiwe amejihusisha na
matumizi ya dawa za kulevya.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekuwa likiwaandaa vijana kujiajiri kwa kuwajengea stadi za maisha na kuwawezesha kuwa wazalendo, waadilifu na walio tayari kulilinda Taifa.
0 comments:
Post a Comment