METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 24, 2017

MHE ANTHONY MAVUNDE ATOA MAHUBIRI KWA VIJANA MTWARA

KON1
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE kitembelea karakana wakati alipozindua  Mafunzo ya UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam mkoani Mtwara.
KON2
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE akizindua Mafunzo ya UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaa.
……………………………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE amezindua Mafunzo ya UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam mafunzo yaliyozinduliwa Mkoani Mtwara. 

Mhe Mavunde amewataka Vijana kuchangamkia fursa wasisubiri serikali itoe matangazo, iwatafute, iwakusanye, iwape ujuzi  Msingi wa maisha ya kijana unaanzia hapa  Kijana wa kitanzania jiamini, timiza wajibu wako 

OMBI KWA VIJANA  Vijana waliopata fursa ya kuingia kwenye Mafunzo Haya, kutumia vizuri fursa hii kwa kuwa WAAMINIFU na KUWAJIBIKA kama msingi wa mafanikio, Waache Tamaa waende kwa Hatua. 

“ni kaburi peke yake watu waanza kuchimba kuanzia juu kwenda Chini, lakini maisha yananzia Chini kwenda juu” amesisitiza Mhe Mavunde. 

Mafunzo haya yanatolewa na Serikali kupitia Fedha za walipata KODI, hivyo wahakikishe wanatumia vizuri fedha zinazotolewa katika mafunzo Haya mana ni fedha za watanzania, Serikali ya Mhe John Pombe Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea UWEZO vijana ili waweze kunufaika na maendeleo ya rasilimali zilizopo nchini. 

Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini 
Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
24/08/2017
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com