Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman (wa pili kushoto) akichangia mada wakati wa kongamano la AISEC lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Kushoto) ni Mtaalam wa Ajira wa ILO, Jealous Chirove,wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trade Mark East Africa (TMEA) John Ulanga, na (kulia) ni Mwanzilishi wa AISEC Tanzania, na Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Lettice Rutashobya.
Meneja Mwandamizi wa TBL ,Raj Chandarana,akiongea na wanafunzi wakati wa maonyesho haya.
Meneja wa Ukuzaji Vipaji wa TBL, Kissa Mwasomola akiongea na baadhi ya wanafunzi.
Meneja Mauzo wa Wilaya,Sylivester Silya akitoa mada kwa wanafunzi.
Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi akitoa mada wakati wa maonyesho hayo.
Maofisa Waandamizi wa TBL wakifuatilia mada wakati wa maonyesho hayo.
Wanafunzi wakifuatilia mada kutoka kwa Maofisa Waandamizi wa TBL.
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL),kwa mara nyingine imeshiriki katika maonyesho ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliyoandaliwa na chama cha AISEC Tanzania na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mlimani.
Kupitia maonyesho hayo wanafunzi huweza kujua jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo kwa kujifunza,kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman,aliongoza jopo la wafanyakazi waandamizi wa kampuni katika maonyesho hayo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya TBL chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV inavyoendesha shuguli zake sambamba na kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Milenia.
0 comments:
Post a Comment