Katika kukuza vipaji vya vijana katika
Mkoani Dodoma, Diwani wa Kata ya Buigiri iliyopo Wilaya ya Chamwino, Mhe
Kenneth Yindi ameandaa mashindano ya Mpira wa Miguu yatakayoshirikisha
Timu Nane za Kata hiyo.
Mashindano hayo yaliyopewa jina la
Buchimwe Cup 2019, yatazinduliwa kesho na Mkurugenzi wa Michezo Nchini,
Ado Komba ambapo mshindi wa kwanza atajnyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi
na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.
” Lengo la mashindano haya ni kukuza
vipaji vya vijana wetu, Michezo imekua Ajira kubwa Duniani kote hivi
sasa, hivyo kama Diwani nimeoana nianzishe mashindano haya ambayo
naamini yatatumika kama fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata Timu
kubwa zaidi ya hizi walizonazo sasa.
‘ Tunashukuru Wizara ya Michezo chini ya
Waziri Mhe Harrison Mwakyembe kwa kutuunga mkono katika kufanikisha
mashindano haya bila kuwasahau Chama Cha Soka Mkoa (DOREFA),” amesema
Mhe Yindi.
Ameongeza kuwa licha ya Ligi hiyo
kuchezwa pia ameandaa mafunzo ya uamuzi kwa waamuzi waliyopo ndani ya
Kata yake yenye viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.
” Kwa kushirikiana na wenzetu wa Dorefa
tumeandaa pia mafunzo haya kwa waamuzi na watakaofuzu watakabidhiaa
vyeti vya kuhitimu, lengo letu ni kukuza Michezo kwenye Mkoa wetu, ”
amesema Yindi.
Amesema kitendo cha Rais Magufuli
kuwaletea ujenzi wa uwanja wa Kisasa wa Michezo uliopo eneo la Nzuguni
ni heshima kwao hivyo hawana budi kuhakikisha sasa wanaandaa vijana
wazawa kukua kimichezo ili kuweza kunufaika na uwanja huo.
” Rais Magufuli tunampongeza sana kwa
kutupa heshima kubwa ya uwanja wa kisasa, sasa ni jukumu letu sisi
wasaidizi wake kuwaandaa vijana wetu kimichezo ili wanufaike na zawadi
hii ambayo Mhe Rais ametupa sisi watu wa Dodoma,”
Mhe Yindi amesema pia kutakua na zawadi
Kwa mshindi wa pili na wa tatu, mfungaji na mchezaji bora wa mashindano,
kipa bora pamoja na mchezaji bora wa kila mechi.
0 comments:
Post a Comment