Na Emmanuel Michael Senny, Kigoma
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Luten
Kanal Michael Ngayalina amewata wananchi kushirikiana kikamilifu na jeshi la
polisi wilayani humo kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili hatua
zichukuliwe mapema.
Kanal Ngayalina aliyasema hayo wakati akizungumza
na wananchi wa kata ya Kajana wilayani humo katika mkutano wa kuhamasisha
ulinzi na usalama wa nyumba kumi kumi na kuongeza kuwa hatavumilia vitendo vya
uhalifu katika halmashauri hiyo.
Aliongeza kuwa mtu yeyote atakaye kamatwa hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na kwa wananchi atakayebainika
akishirikiana na wahalifu nae pia atachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa
wengine.
"Siwezi kukubali wilaya yangu kuwa na matukio
ya kihalifu hivyo basi polisi simamieni hili kikamilifu lakini pia wananchi
muwe mstari wa mbele kutoa taarifa za wahalifu ili kuendelea kulinda amani ya
wilaya na nchi kwa ujumla" alisema Ngayalina.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya
kipolisi Manyovu Buhigwe Omari Mzuza, alibainisha kuwa wananchi walio
wengi wanawaficha wahaifu bila kujua huku akiwataka kuwa wepesi wa kutoa
taarifa kwa kila mgeni anayeingia kijijini.
"Wilaya yetu iko mpakani hivyo tunapokea
wageni wa kila aina na wengi wetu tunapokea na kukaa na wahalifu bila kujua
kwahiyo kabla ya kukaribisha mgeni peleka taarifa kwa uongozi wa kijiji ili
mgeni atambulike na sisi kama polisi tutashughurikia uhalifu wilayani
hapa" alisema Mzuza.
Naye mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kasumo
Damasi Gabriel alisema uwepo wa nyumba kumi za ulinzi na usalama umesaidia
kupunguza uhalifu na kwamba doria za kila siki ndani ya kijiji hicho zimeongeza
uwepo wa amani kwa wananchi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment