METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 18, 2019

WANAFUNZI WA KIKE WATAKIWA KUJIKINGA NA MIMBA ZA UTOTONI MKOANI IRINGA

 Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi  akipokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus wakati wa mahafali ya klub za FEMA yaliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana ya Ifunda mkoani Iringa.
 Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kwenye mahafali hayo ya klabu za FEMA 
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi  akiwa  katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus  pamoja na wageni wengine wakelekea ukumbini kwenye sherehe za mahafali ya klabu za FEMA mkoani Iringa. 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi amewataka wanafunzi wa kike kujikinga na mimba za utotoni ili kujijenga malengo mazuri ya hapo baada yenye tija kwa taifa na wao binafsi.

Akizungumza wakati wa mahafali ya club za FEMA yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Ifunda Girls,Ngowi alisema wanafunzi wengi wa kike huacha masomo mapema kutokana na kupata mimba wakiwa bado wapo masomoni hivyo ni lazima mjijengee malengo.

“nimetembea sehemu nyingi nimekuta nimekutana na watoto wakike wengi wameacha shule kwa sababu ya kupata mimba wakiwa shuleni,hivyo hata nyie mnatakiwa kujitunza na kuwa na maisha mazuri na bora kama ambavyo mnatuana baadhi ya wanawake tunafanya vizuri kwa kuwa  tulijitunza toka tukiwa shuleni” alisema

Ngowi aliwaambia,starehe na mapenzi vipo siku zote za maisha hivyo lazima mjitambue katika umri huu ndio muda wa kutengeneza dira ya maisha yenu hapo baadae kwa faida yenu.

“Kila mwanamke ambaye mnamuna hivi sasa amefanikiwa ni kutokana na kujitunza walipokuwa wanasoma kama ambavyo nyie mpo hivi sasa,mnatakiwa kujifunza kutoka kwa wanawake walifanikiwa”  alisema

 Aidha Ngowi aliwataka wanafunzi kuwa wazalendo na maendeleo ya nchi yao kuwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa kuwapotosha juu ya ukweli ambao unaendelea kwenye nchi hii,hivyo lazima muwe wazalendo wa kweli kwa kuipenda nchi yetu na kuilinda isiingie kwenye machafuko.

“Ili uweze kufanikiwa katika maisha uzalendo ni japo la kwanza na la msingi kabisa kwenu nyie wanafunzi kwa kuwa ndio taifa la sasa na baadae kwa kuwa mtakuja kuwa viongozi wa kuongaza nchi hii na siwa watu wengi hata sisi ni viongozi ambao tulisoma katika shule kama hizi ambazo nyie mnasoma hivi sasa” alisema

Akiwa katika mahafali hayo mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi aliwachangia viongozi shilingi laki mbili kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kufika katika maeneno ambayo wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi hao zaidi ya mia nane wa mkoani Iringa.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi, katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus alisema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendeshea semina mbalimbali wa walimu walezi wa mkaoni Iringa.

“Tunakosa pia fedha za kuendeshea matamasha mbalimbali yenye kubeba ujumbe mzuri katika jamii,ukosefu wa ofisi ya FEMA mkoa wa Iringa” alisema

Tunus alisema kuwa mikakati yao ni kuhakikisha wanaandaa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wananchama wa FEMA yatakayo kuwa yanahusisha shule za sekondari tano za mkoa wa Iringa.

“Tutaendelea kushirikiana na serikali katika kuwalea vijana katika maadili mema na kuhakikisha FEMA klabu zinaenea katika shule zote za sekondari hapa mkopani iringa” alima Tunus


Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com