Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Kumekuwa
na dhana ya kila mkulima wa korosho kulalamika kuwa hajalipwa fedha za korosho zake
jambo hili limeibua sintofahamu katika jamii.
Katika
hali hiyo serikali sasa imeamua kuja na mkakati kabambe wa kubandika majina ya
wakulima wote waliolipwa fedha zao ili kuondokana na kadhia ya lawama za
wakulima wasioitakia mema serikali.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Machi 2019 wakati
akizungumza mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge, Mifugo na Maji kwenye kikao
kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Agizo
hilo limetolewa kwa wataalamu wanaoongoza timu ya Oparesheni Korosho kubandika
majina ya wakulima wote waliolipwa ili kuondoa sintofahamu katika jamii.
“
Mimi nashangaa sana kila mkulima akiulizwa anasema hajalipwa jambo hili sio
sawa nadhani wanafanya hivi kukwepa madeni wanayodaiana huko vijiji, sasa
naitaka timu ya wataalamu wa Oparesheni korosho kuhakikisha majina yote ya
wakulima waliolipwa yanabandiikwa kwenye ofisi za vijiji ” Alikaririwa Mhe
Hasunga
Alisema
kuwa wanapaswa kubandika orodha ya majina ya watu waliolipwa na kiasi cha
korosho walicholipwa.
“Mpaka sasa Tani 222,684 zimekwisha kusanywa huku hadi
kufikia tarehe 14 Machi 2019 tayari jumla ya Shilingi Bilioni 596.9 zilikuwa
zimekwishalipwa kwa wakulima kati ya Shilingi Bilioni 723 lakini nashangaa wakulima
wanasema hawajalipwa hili sio sawa” Alisema Mhe Hasunga
Sambamba na hayo Waziri Hasunga alisema kuwa Serikali imejipanga hadi kufikia tarehe 31 Machi 2019 wakulima wote
watakuwa wamelipwa fedha zao kwani uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli
inapaswa kuungwa mkono kwa maamuzi magumu kwenye korosho kwa kuamua kuwalipa
wakulima shilingi 3300 kwa kila kilo moja ya korosho.
Kadhalika,
ameshangazwa na Mkoa wa Mtwara ambao unazalisha kwa karibu nusu ya korosho zote
nchini lakini imebaini idadi ndogo ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya
Korosho kinyume na sheria maarufu kama kangomba ukilinganisha na mkoa wa Lindi
ambao una idadi kubwa ya Kangomba.
“
Nashangaa sana Mkoa wa Mtwara una Kangomba 10 lakini ndio wazalishaji wakubwa
wa korosho huku Mkoa wa Lindi ambao unafuatia kwa uzalishaji wa korosho ukiwa
na idadi kubwa ya Kangomba ambao wapo zaidi ya 400” Alisema
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
Mhe Dkt Christine Ishengoma amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwa
kuanzisha zoezi la usajili wa wakulima nchini.
“
Nakupongeza sana Waziri Hasunga kwa hili lakini hakikisha unalisimamia kwa
weledi jambo hili ili liwe na matokeo chanya na wakulima waweze kutambulika
kote nchini kwani kufanya hivyo serikali itakuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa
ufasaha” Alisema
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiongozwa na Mhe Dkt
Christine Ishengoma wameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara
wakikagua miradi ya maendeleo katika sekta husika za Kilimo, Mifugo na Maji.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment