Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya I CAN ya heshima kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation Dkt. Reginald Mengi (kushoto) kwa kutambua mchango wake katika kusaidia watu wenye ulemavu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Watu wenye Ulemavu waliohudhuria hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha juu kitabu cha I Can, I Must, I Will kama ishara ya kuzindua toleo maalum kwa wasioona (kiatu cha nukta nundu) leo wakati wa hafla ya utoaji tuza ya I CAN pamoja na chakula cha mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza watu wenye ulemavu
kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.
Makamu wa Rais ameyasema
hayo leo kwenye hafla ya utoaji tuzo ya I CAN kwa watu wenye ulemavu
iliyoandaliwa na Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi Foundation, iliyofanyika leo kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
“Serikali
inapenda kuwahakikishia kuwa changamoto za walemavu zinafanyiwa kazi moja baada
ya nyingine.”Alisema Makmu wa Rais.
Aidha, Serikali imeendelea
kuweka mifumo, taasisi mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha
kuwa kuna miundombinu wezeshi ya elimu, afya na teknolojia ili watu wenye
ulemavu kuajirika kwenye viwanda vyetu.
“Nitoe rai kwa
waajiri na wamiliki wa viwanda kote nchini kuhakikisha kuwa hawabagui wala
kunyanyapaa walemavu katika kuijenga Tanzania ya Viwanda ambayo ni jumuishi kwa
wote” alisisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema
Serikali inatambua, inathamini na inapongeza jitihada za Dkt. Reginald Mengi
pamoja na taasisi yake mpya ya Dkt. Reginald Mengi Persons with Disabilities
Foundation ambayo pamoja na mambo mengine inahimiza ujumuishwaji wa watu wenye
ulemavu katika ajira.
Vilevile Makamu wa Rais
aliwaambia wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa Serikali imeweka mkazo maalum
katika masuala ya elimu jumuishi ambapo watu wenye ulemavu watasoma vizuri
kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
Kwa Upande mwingine Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema Tuzo za I CAN zimekuwa chachu sana kwa watu
wenye ulemavu ambapo alimpongeza na kumshukuru Dkt. Reginald Mengi kwa moyo
wake wa kipekee wa kutambua na kuwasaidia walemavu.
Aidha, amesema Serikali ina
mpango endelevu wa kutoa elimu ya masuala ya ulemavu ikiwa pamoja na
kuendelea kufanya jitihada za kuongeza wakalimani wa lugha za alama.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema sera ya elimu na mafunzo ya
mwaka 2014 inatambua fursa na haki sawa katika kupata elimu hivyo Serikali
inaendelea kuboresha miundombinu wezeshi kwa wote wenye mahitaji maalumu.
0 comments:
Post a Comment