METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 21, 2020

CHAMA CHA MAPINDUZI CHATOA SIKU 30 KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILINDINI – MICHEWENI, KASKAZINI PEMBA




CHAMA cha mapinduzi chatoa siku 30 kukamilishwa kwa mradi wa maji kilindini - micheweni, kaskazini pemba 

akiwa katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya ya Micheweni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimetoa siku 30 kukamilishwa kwa mradi wa maji Wilaya Micheweni Pemba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Polepole kufika katika eneo la Kilindini ambapo kuna chanzo cha maji kinachopasa kupeleka maji kwa kilometa 4.6 hadi eneo la Micheweni lakini mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na kuelekeza kukamilika kwa haraka kwa mradi huo wa maji ili kurahisisha huduma za kijamii na Kiuchumi katika Wilaya ya Micheweni.

Aidha Ndugu Polepole ametembelea katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kije iliyopo Jimbo la Wingwi, Wilaya ya Micheweni na kueleza kuwa ujenzi wa skuli hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba shule hiyo ni mojawapo ya miradi iliyojengwa kama ziada ya utekelezaji mzuri wa ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Wakati uo huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Maji tayari imetoa pampu itakayofungwa katika eneo la kilindini na itasafirishwa kesho kwenda kisiwani Pemba.

Huu ni muendelezo wa ziara za kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ili kuhakikisha kila liloahidiwa na CCM linatekelezwa kwa wakati, ufanisi, ufasaha, ubunifu na maarifa zaidi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com