Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa maazimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyikia katika kata ya ulanda mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali akiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA) ambao ndio wamesaidia kutoa hati miliki kwa wanawake na kupunguza migogoro wilaya ya Iringa
Wadau wakiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA)
Na Fredy Mgunda, Iringa
Na Fredy Mgunda, Iringa
WANAWAKE mkoani Iringa
wametakiwa kuanza kumiliki ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo
na badala yake waachane na tamaduni kandamizi za kuwaachia wanaume katika
umiliki wa mali.
Akizungumza kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela katika kilele cha maadhimisho ya
wanawake yaliyofanyika katika kijiji cha ibangamoyo kata ya ulanda wilaya ya
Iringa alisema kuwa wanawake waaze kumiliki ardhi ili kujiinua kiuchumi kwa
kuwa wanawake ndio walezi wa familia tofauti na wanaume wanaokuwa na makazi
tofauti tofauti.
Kasesela aliwataka wanaume
kuwapa haki wanawake kumiliki ardhi kwa kuwa wanahaki hiyo kwa mujibu wa sheria
na kanuni za nchi hivyo mwanaume atakayemkataza mwanamke kumiliki ardhi
atachukuliwa hatua za kisheria.
“Nasema nileteeni wanaume
wote wanaowazuia wanawake kumiliki ardhi tutamtafutia sehemu ya kuishi kwa kuwa
atakuwa anakiuka katiba ya nchi yetu hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake”
alisema
Akitembelea banda la mradi
wa urasilmishaji ardhi vijijini (LTA), Kasesela alisema kuwa mradi huo umekuwa
mkombozi kwa wanawake kumiliki ardhi kutokana na kutoa elimu kwa wanaume na
kufanikisha wanawake kupatiwa hati miliki za kimila ambazo ndio limekuwa
suluhisho la migogoro ya ardhi vijijini.
Aidha Mtaalam wa mawasiliano
na uenezi wa mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA), Jackline Mhegi alisema
kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasisitiza kuwa
binadamu wote ni sawa na huzaliwa huru hivyo
basi wanatakiwa kupata ulinzi sawa na sheria za nchi ikiwepo kumiliki ardhi.
“Kwa mujibu wa ibara ya
24(I) inasema kila mtu anahaki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali
yake aliyokuwanayo kwa mujibu wa sheria,hivyo mwanamke ana haki ya kumiliki
ardhi kama mojawapo ya mali na kupata ulinzi wa mali kulingana na katiba ya
nchi” alisema Mhegi
Mhegi alisema, sera ya taifa
ya ardhi ya mwaka 1995 inaeleza kuwa “ni haki ya kila mwanamke
kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kugawa ardhi kwa kuwa hata mwanaume ana haki hiyo” Sheria
ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999,Kwa mujibu wa kifungu cha 3 (2) cha Sheria
ya ardhi Na.5 ya Vijiji ya mwaka 1999 inasema “Haki ya kila mwanamke kupata,
kumiliki, kutumia na kuuza au kuigawa ardhi ifahamike kuwa ni sawa na haki ya
mwanamume yeyote kwa viwango vilevile na masharti yaleyale”
“Sheria
hizi zimeondoa ubaguzi dhidi ya mwanamke. Mwanamke anaehitaji ardhi atafuata
taratibu zinazohusika na hapaswi kunyimwa ardhi kwa sababu tu yeye ni mwanamke,
Sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2002, Sheria ya
marekebisho ya utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2004, Sheria ya ndoa ya
mwaka 1971”alisema Mhegi
Mhegi alimalizia kwa kusema,
Wanawake ni watumiaji wakuu wa ardhi hivyo vyombo vinavyohusika na masuala ya
usimamizi na utawala wa ardhi vihakikishe kuwa wanawake na wanaume
wanashirikishwa ipasavyo katika masuala yahusuyo ardhi ili kuleta usawa wa
kijinsia katika usimamizi na umiliki wa ardhi utakao changia maendeleo endelevu
kutoka na rasilimali ardhi kiuzalishaji, Hivyo wanawake wahakikishe wanatumia
nafasi walizonanzo kwa kushiriki na kutoa mawazo yao kwa lengo la kuboresha
maslahi ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Naye
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Stella Mosha,
alisema ni wakati sasa kwa wanawake kutambua ya
kwamba wana haki ya kumilki ardhi sawa kama wanavyomiliki wanaume kwa njia
mbalimbali zikiwemo wao binafsi, wao Pamoja na waume au ndugu zao.
“Pia jamii inakumbushwa kuachana na mila na desturi kandamizi
katika zinazo wazuia wanawake kuto miliki ardhi kwa sababu wakati umebadilika
wanawake na wanaume wanatakiwa kushirikiana ili kuweza kuinua uchumi wa familia
na baadae taifa kwa ujumla” alisema mosha
Mosha
aliesma,Mradi uliweza kutoa elimu ya juu ya haki ya wanawake kupitia mikutano
ya hadhara kwa kila kijiji kwa wanawake pekee na baadae kuwaunganisha na
wanaume ili kuwa na majadiliano ya pamoja.
“Mradi
ulitoa mafunzo juu ya Sera na Sheria za ardhi zinazoelezea haki ya wanawake
kumiliki rasilimali ardhi” alisema mosha
Mosha
alimalizia kwa kusema,mradi uliwajengea uwezo wanawake kuingia katika vyombo
mbalimbali vinavyosimamia masuala ya usimamizi wa ardhi ngazi ya kijiji, kama
vile: kamati ya Mpango bora wa Matumizi ya ardhi, Kamati ya Uhakiki wa maslahi
ya ardhi, Baraza la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya kijiji.
0 comments:
Post a Comment