
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Wambi mjini Mafinga, Septemba 26, 2019

Viongozi wa Dini wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara
kwenye Uwanja wa Wambi mjini Mafinga, Septemba 26, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwapungia wananchi wakati aliowasili kwenye uwanja wa Wambi mjini
Mafinga kuhutubia mkutano wa hadhara, Septemba 26, 2019.

Wananchi wakimshangili Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye
uwanja wa Wambi mjini Mafinga, Septemba 26, 2019.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
……………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya
Mji wa Mafinga wahakikishe wanajenga mradi wa kimkakati kwa kutumia
fedha za mapato ya ndani na si kusubiri miradi kutoka Serikali Kuu
wakati wanakusanya zaidi ya sh. bilioni saba kwa mwaka.
Amesema halmashauri hizo licha ya
kukusanya fedha nyingi kwa mwaka lakini matumizi yake si mazuri kwa
sababu hawana mradi wowote wa kimkakati wanaoutekeleza, mfano ujenzi wa
maeneo ya kuegeshea magari makubwa au hata ujenzi wa kituo cha mabasi,
miradi ambayo ingewaongezea mapato.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana
jioni (Alhamisi, Septemba 26, 2019) wakati akihutubia na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Wambi wilayani
Mufindi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.”Nataka kuona
mradi wa kimkakati ukitekelezwa kwa fedha mnazokusanya kutoka kwa
wananchi.”
Alisema viongozi hao wanaweza
kutenga kiasi cha sh. bilioni moja kwa mwaka na kujenga hospitali au
wakatenga fedha na kujenga barabara za lami kwa awamu katika Halmashauri
ya Mji wa Mafinga kwa kuwa ujenzi wa barabara za lami mijini ni sh.
milioni 300 kwa kilomita moja, hivyo wangeweza kutekeleza ujenzi huyo
kutokana na fedha wanazokusanya.
“Msitegemee fedha kutoka Serikali
Kuu tu jengeni wenyewe barabara zenu kuzunguka Mji wa Mafinga kwa
kiwango cha lami kwa sababu mna fedha za kutosha tena mnaweza kutumia
fedha za mapato ya ndani mnazokusanya kutoka kwa wananchi badala ya
kuzitumia kwa kulipana posho tu.”
Awali,Waziri Mkuu alitembelea
shule ya Sekondari ya kata ya Mdabulo na kupokea taarifa fupi ya ujenzi
wa bwalo, bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike pamoja na ujenzi wa
madarasa na kisha alizungumza na wananchi na kuwaeleza miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao.
Waziri Mkuu alisema katika
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na maeneo yao
ya makazi, Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya afya katika
kila kata pamoja na ujenzi wa hospitali za wilaya ikiwemo na wilaya yao
ya Mufindi ambayo ipo katika hatua mwisho kukamilika.
Kwa upande wao, wabunge wa mkoa wa
Iringa wakiwemo wa majimbo na wa viti Maalumu kwa nyakati tofauti
waliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
kwenye mkoa wao.
0 comments:
Post a Comment