Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Miss Uganda 2018
ambaye pia ni Miss World Africa Quiin Abenakyo (kulia) wakati wa mkutano wa
Africa Now Summit 2019 unaofanyika Munyonyo, mjini Kampala, Uganda. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ili
kuibadili Afrika Viongozi wake lazima wawekeze kwa Vijana na Watoto.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now
Summit 2019 jijini Kampala nchini Uganda.
“Viongozi lazima wahakikishe wanawekeza kwenye lishe bora ya watoto
wanaozaliwa na kuhakikisha mifumo yetu ya elimu inalenga katika kutoa elimu
bora na zenye kukuza vipaji ili kwenda sawa na ulimwengu wa teknolojia.”alisema Makamu wa Rais.
Aidha
Makamu wa Rais amesisitiza Afrika lazima iwekeze kwenye mipango itakayoleta
maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo na si mipango kwa ajili ya chaguzi
zijazo.
Mkutano
huo uliofunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni unalengo la
kuwakutanisha Viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali ya utengamano
katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.
Rais
Museveni amesema kwa kipindi kirefu Afrika haijabadilika ni wakati wa kuboresha
elimu, kuboresha bidhaa zinazoingia sokoni, kupanua soko la kimataifa ambalo
kwa sasa limeonekana finyu na kuimarisha miundombinu na kutambua umuhimu wa
Sekta Binafsi katika kuleta mabadiliko endelevu ya kiuchumi.
Viongozi
wengine walioshiriki wakati wa ufunguzi ni Rais wa Somalia Mhe. Mohamed
Abdullahi Mohamed, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto na Waziri wa Biashara na
Viwanda wa Misri Mhe. Amr Nassar.
0 comments:
Post a Comment