Mtandao wa Jinsia nchini TGNP wajivunia mafanikio waliyopata kupitia miradi mbali mbali ilioanzishwa chini ya shirika hilo yenye lengo
la ukombozi kwa mtoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya washiriki wakiangalia picha mbalimbali za ukatili wa kijinsia pamoja na uwezeshaji wanawake na wasichana katika tafrija iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Akitoa ufafanuzi kupitia njia ya picha kwa washiriki wa semina hiyo mapema jana jijini Dar es salaam Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa Mtandao huo Bi. Anna Sangai amesema kuwa miradi iliyoanzishwa
kupitia Mtandao huo imeweza kumuokoa mtoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji
na unyanyasaji katika jamii na kumfanya aweze kuishi kwa kujiamini.
“Kiukweli miradi hii imeweza kuokoa watoto wa kike dhidi ya
kufanyiwa ukatili ukiwemo wa ndoa za utotoni, Ukeketaji na kudumazwa
kiuchumi, hasa tukitazama mradi wa Kipunguni ambao wanaharakati wameanzisha shughuli zao za kiuchumi na kumsaidia
mtoto kuondokana na utegemezi”.alisema Sangai
Aidha,katika hafla hiyo iliyobeba kauli mbiu ya” AKEKETWI
MTU, Mlinde mtoto wa kike dhidi ya ukatili ”baadhi ya viongozi wakiwemo madiwani na wabunge kutoka sehemu mbali mbali
walialikwa na kupata nafasi ya kutoa neno la kuwatia moyo wanaharakati kuwa
wanaweza kufika wanapopataka kama watatia nia katika harakati zao.
“Niwatie moyo wanawake wenzangu mimi mwenyewe ni mmoja kati
ya walionusulika kufanyiwa ukatili huo lakini nilisimama katika maamuzi ya
kuhitaji kusoma na mpaka leo ni kiongozi japo nilipitia changamoto nyingi”.alisema
Catheline Ruge,Mbunge viti maalumu mkoani mara.
Pia,Wanaharakati wamepongeza jitihada ambazo TGNP mtandao unazifanya katika
kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya madhala yatokanayo na ukatili wa
kijinsia kwa mtoto wa kike ikiwemo ukeketaji, Ndoa za Utotoni, Unyanyasaji na mengine huku wakihaidi kuendeleza harakati
mpaka mtoto wa kike atapokombolewa kutoka katika ukatili huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao akitoa ufafanuzi kuhusiana na tafrija hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakijadili jambo fulani katika Maonesho ya picha za Mashujaa wa ukeketaji yaliyofanyika ofisi za shirika hilo mapema jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia tafrija.
0 comments:
Post a Comment