METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, December 23, 2018

MHE HASUNGA APONGEZA UZALENDO WA WALIMU

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa kilimo akizungumza kwenye kikao na baadhi ya walimu wa mkoa wa Songwe kilichofanyika katika kata ya Vwawa tarehe 23 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya walimu Mkoani Songwe wakifatilia kwa makini maelezo ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa kilimo wakati akizungumza kwenye kikao na baadhi ya walimu wa mkoa wa Songwe kilichofanyika katika kata ya Vwawa tarehe 23 Disemba 2018
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao na baadhi ya walimu wa mkoa wa Songwe kilichofanyika katika kata ya Vwawa tarehe 23 Disemba 2018.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa kilimo akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa mkoa wa Songwe mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika kata ya Vwawa tarehe 23 Disemba 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa kilimo amewapongeza walimu kwa uzalendo wanaouonyesha katika uwajibikaji wao katika kuhakikisha Taifa linasonga mbele kielimu.

Mhe Hasunga ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka katika shule mbalimbali za Mkoa wa Songwe kilichofanyika katika kata ya Vwawa.

Katika mkutano huo mbunge huyo ameridhia ombi la kuwa mlezi wa walimu hao katika mkoa wa Songwe ambapo ameahidi kushirikiana kwa hali na mali ili kutatua changamoto zinazowakabili walimu katika mkoa huo.

Alisema kuwa walimu wanapaswa kuheshimiwa kwani wanafanya kazi kubwa ya kuongeza weledi kwa wanafunzi nchini ambapo wasomi hao ndio muhimili wa Taifa.

Alisema pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakumba walimu ambazo zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi na serikali lakini wameendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi uliotukuka.

Katika kikao hicho walimu wameomba kutatuliwa changamoto sugu ambazo ni pamoja na upandishaji wa madaraja, mapunjo ya mshahara, sambamba na fedha za likizo na matibabu.

MWISHO.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com