Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline S.L Mabula kwa niaba ya familia amewashukuru ndugu, jamaa, marafiki na viongozi mbalimbali kwa kuungana na kuifariji familia ya marehemu katika kipindi kigumu cha kufiwa na Mzee wao Sylvester Lubala
Dkt Angeline Mabula pia ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wale wote waliojitolea huduma ya usafiri wa kusafirisha waombolezaji kutoka Dar es salaam kwenda mkoani Mwanza na kutoka Mwanza mjini kwenda mazikoni Sumve, waliojitolea huduma ya chakula, waliojitolea huduma ya maji ya kunywa na wengine kwa michango yao mbalimbali iliyosaidia kufanikisha shughuli za mazishi sambamba na kuwaomba kuendelea kufanya hivyo kwa watu wengine watakaopatwa na matatizo ya namna hiyo ili kuendelea kuimarisha mahusiano na kusaidia jamii kwa upana wake
Mzee Sylvester Lubala amezikwa kijijini kwake Bumyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba April 14, 2018
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI, AMINA
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
18.04.2018
0 comments:
Post a Comment