METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, January 20, 2018

Dkt Mwigulu Aagiza wananchi kushirikiana na serikali ujenzi vituo vya Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi kushirikiana na serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la ulinzi ni ajenda ya kila mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele.

Akizungumza na wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Dk Mwigulu alisema kuwa mkakati wa halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa cha polisi ni cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina zote.

Alisema maeneo mengi nchini yanahiotajika vituo vya polisi na kwamba serikali pekee haiwezi kujenga vituo hivyo kwa siku moja badala yake wananchi na wadau wanaweza kusaidia ujenzi huo.

*‘’Ujenzi huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama kwani bado kunahitajika vituo vingi zaidi hapa nchini na serikali haiwezi kujenga kwa siku moja. Wizara itaangalia namna ya kuwasaidia kwenye ujenzi huu name nitatoa nondo 500, mifuko ya saruji 500 na fedha za mafundi,’’ alisema Dk Mwigulu.*

Aidha, amelitaka jeshi la polisi kutafuta namna ya kurekebisha wahalifu wanaokamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uzururaji ili kupunguza mrundikano katika mahabusu.

Alisema kuwa *ipo haja ya kuangalia utaratibu wa urekebishaji wa watuhumiwa wa makosa hayo ili wasiweze kupata nafasi ya kuzungumzia masuala ya uhalifu na watuhumiwa waliozoea.*

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com