Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas
(kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Meneja
Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen
Adili (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali
ya benki hiyo ambayo ni moja ya mdhamini wa mkutano huo.
Mwanahabari na Blogger Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger
Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mablogger kazini.(P.T)
Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence Mello akitoa mada.
Meza kuu.
Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Kranty
Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki
ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji
wa Serikali Dk. Hassan Abbas, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi
pamoja na Katibu wa muda wa TNB, Khadija Kalili.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Bloggers wakifuatilia mada.
Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akihutubia.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger
kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni
William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki
wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.
Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa
Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).
“Serikali
sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari
kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya
habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa
mbalimbali” alisema Abbas.
Abbas
alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka
mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi
sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.
Katika
hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine
hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi
vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo
vingine.
Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.
Wanamitandao
hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo
kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja
na kunyimwa ‘Press Card’ jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
0 comments:
Post a Comment