METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, January 19, 2018

TIMU YA UFUATILIAJI MIRADI TAMISEMI YAIPONGEZA MANISPAA YA ILEMELA

Timu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya afya kutoka Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeipongeza halmashauri ya manispaa ya Ilemela kwa ujenzi uliozingatia ubora na ufanisi wa majengo ya kisasa ya kituo cha afya cha Karume kilichopo kata ya Bugogwa manispaa ya Ilemela.

Pongezi hizo zimetolewa na kiongozi wa Timu hiyo ndugu Rasheed Maftah ambae pia ni mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Karume na kukagua ujenzi wa kituo hicho akiambatana na wataalamu wengine kutoka ofisi yake ambapo amesema anaridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho uliozingatia ubora na viwango vya kitaalamu vinavyotakiwa kwa kutumia mafundi wa kawaida mtaani uliosaidia kupunguza gharama na kukamilika haraka  kwa mradi

‘…Kiukweli niseme tu ripoti ya ujenzi ni nzuri na tumeona uhalisia hapa inaonesha kweli thamani ya pesa inaonekana na maelekezo ya katibu mkuu kwa kiasi kikubwa mmeyazingatia, nawapongeza saana …’ Alisema

Kwa upande wake msanifu majengo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza ndugu Chagu Nghoma amezitaja changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelzaji wa miradi ikiwemo uhaba wa baadhi ya malighafi za ujenzi na uvamizi wa maeneo ya umma kitendo kinachozalisha migogoro isiyo ya lazima na kuchelewesha miradi hiyo  hivyo kuwaomba kuzitafutia ufumbuzi wa haraka changamoto hizo.

Nae  mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ndugu John Wanga mbali na kushukuru kwa pongezi hizo ameongeza kuwa mafanikio ya mradi huo ni ushirikiano mzuri uliopo katika manispaa yake kwa  wataalamu, viongozi na wananchi kushirikiana kwa pamoja huku akiwaasa wananchi kuacha kuvamia maeneo ya umma na kuomba kupungua kwa gharama za upimaji na hati miliki ya ardhi kwa taasisi za serikali ikiwemo masoko shule na vituo vya afya.
Akihitimisha mwenyekiti wa mtaa wa Bugogwa ndugu Alphonce Bundege ameiomba timu hiyo kufikisha salamu za shukrani na pongezi kutoka kwa wananchi wa mtaa wake kwenda kwa Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi huo 

Timu hiyo pia ilitembelea jengo la dharura la hospitali ya wilaya ya Ilemela lililopo kata ya Buswelu kabla ya kwenda kituo hicho cha afya Karume

‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’

19.01.2018

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com