Na. Bornwell Kapinga, Dar es Salaam.
"Mwendo kasi" ni neno lililopata umaarufu mkubwa nchini Tanzania mara tu baada ya kuanza mradi wa usafiri wa haraka *Jijini Dar es Salaam au Jiji la Makonda* ujulikanao kwa lugha ya ng'ambo "Dar Rapid Transit" wenye lengo Mahususi la kupunguza foleni katika Jiji hilo.
"Awamu ya tano ya Uongozi" hapo nazungumzia uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Dr John Pombe Maguli* ambaye kutokana utendaji wake toka awali amekuwa na majina kama "Shining star of Africa", "chuma" ,"Tingatinga" na kazalika.
Utendaji kazi na umahiri wa Mhe.Rais umepelekea kufanya uteuzi makini wa viongozi katika ngazi mbalimbali nchini Tanzania kupitia uteuzi wake makala yangu inaangazia *Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo*.
Manispaa ya Ubungo ndio kwanza ina takribani mwaka mmoja chini ya Mkurugenzi kijana *Ndg John L.Kayombo*
Kijiografia Manispaa hiyo ina miinuko na mabonde na kwenye milima hiyo ndiko yaliko makazi ya watu wengi, sasa ziko changamoto za kimiundombinu.
Wakazi wa maeneo hayo huhitaji kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili kufuata mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ili kuweza kuvuka hukutana na mito au mikondo ya maji.
*Kayombo* katika Manispaa ya Ubungo ameiona changamoto hiyo na tayari kwa kasi ileile ya "zaidi ya Mwendokasi" inafanyika katika maeneo yafuatayo:
Msumi kwa londa: katika eneo hilo lililoko kata ya Mbezi wakazi wake walikuwa na changamoto kubwa ya kuvuka toka upande mmoja kwenda upande wa pili hasa nyakati za mvua kwa sasa daraja la kisasa kabisa linajengwa muda si mrefu itakuwa historia.
Kimara saranga-Upendo kuna kivuko cha waenda kwa miguu: ukiingia ndani kidogo liko eneo tata ambalo nalo wakazi wake wamekuwa wakipata shida ya kuvuka tayari kivuko cha kisasa kinajengwa.
Aidha Manzese kuna kivuko cha kilimahewa cha waenda kwa kwa miguu: licha ya kuwa makazi holela kwa muda mrefu upo mkondo wa maji ambapo wakazi wake wamekuwa wakipata shida ya kuvuka tayari kivuko kimejengwa.
*Ubungo tumejipanga kuboresha maisha wananchi ungana nami kila wiki nikikuangazia masuala anuai yanayofanywa Manispaa ya Ubungo*
0 comments:
Post a Comment