Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi mbalimbali ofisini kwake juu ya kusambaa kwa habari ambayo ilitungwa na mtu mmoja
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Siku chache baada ya
kusambaa kwa picha zinazomuonesha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
akiwa ameshika viungo bandia vya kiume na kuzua Taharuki katika jamii, Mkuu
huyo wa Wilaya ametolea ufafanuzi.
Akizungumza na Wandishi wa
habari ofisini kwake leo Kasesela amesema kuwa taarifa zilizosambaa mtandaoni
juu ya uzalishaji wa viungo bandia vya kiume, zimeleta changamoto huku
akiwataka wananchi kuondokana na dhana
potofu za kuchukua habari za mitandaoni na kuupotosha umma.
“Naomba niendee kuwaomba
radhi watanzania kwa ajili ya jambo ambalo lilileta taharuki kwenye mitandao ya
kijamii hasa nchi ya jirani zetu hapo Kenya lilipokelewa tofauti na nilivyokuwa
hapo awali” alisema Kasesela
Kasesela aliwataka
watanzania kuacha kufuatia mambo ya ajabu na kuyapa nafasi kwenye mitandao ya
kijamii kuliko kupata mambo ya kujenga nchi na yenye tija.
“Jamni ile habari ilitungwa
na ni habari ya hovyo sana kwa kuwa nililishwa habari ambayo mimi sijaisema
kwenye chombo chochote kile kwenye vyombo vya habari hivyo hiyo habari ni ya
kupuuza tu” alisema Kasesela
Kasesela amewashauri
watanzania kuhakikisha wanafatilia taarifa zenye kuleta maendeleo na zenye
kujenga katika jamii inayomzunguka.
“Kwa sasa habari nyingi
ambazo zinazungumzwa hivi sasa ni habari ambazo ni za hovyo hovyo mno ndio
maana leo wamesema kuwa wilaya ya Iringa kuna kiwanda hicho kitu ambacho sio
kweli” alisema Kasesela
Katika hatua nyingine Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela amelaani kitendo cha Dawson Kagine kusambaza taarifa zisizo za kweli na kuongeza
kuwa mkoani Iringa kuna kiwanda cha kuzalisha vifaa vya elimu ya mapambano
dhidi ya Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment