Na mwandishi wetu, Njombe
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imesema ipo tayari kusaidia
uwekezaji kwa
ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya
usindikaji wa Matunda kwa ajili ya kuongeza thamani kwa wakulima wa
matunda wa Mkoa wa Njombe ili kukidhi masoko.
Wito
huo umetolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rehema
Twalib wakati akizungumza
na Umoja wa Wakulima wa Wanajombe AMCOS wakati wa Ziara ya kutembelea
miradi ya kilimo inayowezeshwa na Benki ya Kilimo Mkoani Njombe.
Bibi Twalib alisema kuwa TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa
katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo
nchini hasa kwa wakulima wadogo kwa lengo la kusaidia upatikanaji na
utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya
kilimo nchini.
“Benki imejipanga katika kusaidia kuchagiza
kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini kwa wakulima mkoani Njombe na Tanzania kwa ujumla,” alisema.
Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo ipo tayari kusaidia kukabiliana
na mapungufu katika uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa Matunda kwa ajili ya kuongeza thamani.
Kwa upande wake Mrajis Msaidizi wa Ushirika wa Mkoa wa Njombe,
Bw. Exaud Sepali alisema kuwa Wananjombe wanataka kutumia fursa za mikopo nafuu kutoka Benki ya Kilimo ili waweze kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha kuwa
uendelezaji wa viwanda vya kusindika mazao unafanyika kwa uhakika.
“Fursa
za mikopo ya TADB inatupa nafasi ya kupewa mkopo kwa ajili ya kupata
mtaji kwa ajili ya uendeshaji,
uongezaji wa thamani na gharama za uhifadhi na masoko zitakazotuwezesha
kujenga viwanda vya kusindika matunda ambayo yanalimwa kwa wingi mkoani
Njombe hali itakayotuhakikishia uendelezaji wa wakulima wetu,” alisema.
Naye,
Meneja Ufuatiliaji na Tathamini ya Mikopo wa TADB, Bw. Dickson Pangamawe alisema kuwa
kwa upande wa miundombinu ya masoko, Benki ya Kilimo
inatoa mikopo kwa minyororo ya thamani kwa ajili ya maendeleo ya
miundombinu ya masoko kama vile ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mahindi
na miundombinu ya masoko na kugharamia usafirishaji
wa malighafi na nmatunda yaliyoo tayari kwenda sokoni.
Aliongeza
kuwa Mnyororo wa thamani wa Kilimo cha Matunda ni miongoni mwa
minyororo ya mwanzo inayopatiwa
mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali. Maeneo
yanayowekewa mkazo kwenye Mnyororo wa thamani wa Kilimo cha Matunda ni
pamoja na Uongezaji Tija wa Kilimo cha Matunda na Miundombinu ya masoko.
“Pia
Benki inagharamia uanzishaji wa mifumo ya upatikanaji wa taarifa za
masoko pamoja na kuwezesha
uhusiano wa masoko ya ndani na masoko ya kikanda na kugharamia mahitaji
mengineyo ya kuwezesha miundombinu ya masoko,” aliongeza Bw.
Pangamawe.
Aliongeza
kuwa Dira ya Benki ya kilimo ni kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika
kuleta mapinduzi
ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha
kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza
umaskini.
0 comments:
Post a Comment