Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (wa pili kulia)akifanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha
Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo, Komredi Gennady
Zyuganov (wa pili kushoto) alipomtembelea leo ofisini kwake katika
maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi Makuu ya Urusi. Mheshimiwa Spika
yupo nchini Urusi, akishiriki Mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge
Duniani unaoendelea leo Jijini St. Petersburg, Urusi
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kushoto) akivishwa nishani maalum ya maadhimisho ya miaka 100 ya
Mapinduzi Makuu ya Urusi na Kiongozi wa Chama cha kikomunisti cha
Urusi, Komredi Gennady Zyuganov ambae ni Kiongozi wa Chama cha
Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo alipomtembelea
ofisini kwake. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo akishiriki Mkutano wa
137 wa Chama cha Mabunge Duniani.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job
Ndugai (kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti
cha Urusi na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo Komredi Gennady Zyuganov
(katikati) alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Balozi wa Tanzania
nchini huko, Jenerali Mstaafu Wynjones kisamba. Mheshimiwa Spika yupo
nchini humo kushiriki mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.
PICHA NA OFISI YA BUNGE
0 comments:
Post a Comment