METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, November 1, 2017

KAMPENI YA WANAWAKE NA ARDHI YAZIDI KUWAFIKIA WATU WENGI ZAIDI

Katika kuendelea na kampeni ya Wanawake na Ardhi wadau mbalimbali wamekutana jijini Dar es salaam kujadili juu ya 'Nafasi ya Wanawake katika Michakato ya usimamizi wa ardhi' warsha iliyowahusisha wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Mashirika na wawakilishi wa wakulima na wafugaji.
Kwa ujumla warsha hiyo ililenga malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kuelewa michakato ya mabadiliko mbalimbali ya taratibu za usimamizi wa Ardhi(Mfano marejeo ya sera ya Taifa ya ardhi) na athari chanya au hasi kwa wanawake wa Tanzania,kusambaza ujumbe wa kampeni ya wanawake na ardhi kama ulivyokusanywa kutoka kwa wadau ambao ni wakulima wadogo wanawake,wafugaji na mashirika mbalimbali, pia kupata fursa ya kuipatia Serikali maoni ya wanawake katika marejeo ya sera ya ardhi ya Taifa.

 Bi. Wiyagi Kisandu kutoka WLAC akitoa mada juu ya uelewa wa maswala ya kijinsia kwa jamii na wanawake kwa ujumla, ambapo alisema kuwa ni muhimu Serikali na wadau wengine washirikiane kuwapa elemu ya haki miliki ya ardhi ili iwe rahisi hata kipindi cha mchakato wa kushughulikia kupata hati hizo uwe rahisi.
 Bi. Naomi Shardrack Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Shirika la Kimataifa la Oxfam akielezea kuhusu dhana ya kuwawezesha wanawake kumiliki rasilimali ardhi, pia alielezea utafiti wa maswala ya umiliki wa ardhi uliofanywa na shirika la Oxfam na namna mifumo dume inavyo wakandamiza wanawake katika kumiliki Ardhi.
 Bw. Stephano Mpangala kutoka RUDI akielezea kisa mkasa kilichohusu mzee Kuzenza Magoso(80) ambaye alikuwa na wake sita(6), kwa kutambua umuhimu wa hati milki ya ardhi aliwapatia  wake zake wote hati za kumiliki ardhi ili kuondoa migogoro ambayo ingeweza kujitokeza mbeleni.
Bi.Elisa Simioni   Aliyewahi kushiriki shindano la Mama wa chakula linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la  Oxfam Tanzania akieleza kisa mkasa cha  namna akina amama  walivyoweza kushiriki kikamilifu katika kupigania na kurejesha msitu  kijijini kwao ambao ulivamiwa na kutumika vibaya
 Bw. Adam Ole Mwarabu akielezea zaidi juu ya Kisa mkasa alichozungumzia Bi. Elisa Simion kuhusu uharibifu wa misitu na kusisitiza kuwa licha ya akina mama hao kupigania msitu isiharibiwe, lakini pia akina mama takribani 100 walikwenda kulala katika msitu huo kwa lengo la kuonesha kuwa hawakufurahishwa na uharibifu huo, na mpaka sasa hakuna tena wavamizi katika eneo hilo.
 Bi. Rehema Abdallah mhamasishaji wa umiliki wa ardhi kwa wanawake, alisema kuwa wao wapo tayari katika kushiriki kuchangia gharama za mchakato wa kuhakikisha wanapata hati miliki za ardhi kwa kuwa ni kitu cha muhimu.
 Mh. Yannick Ndoinyo  Diwani wa kata ya Ololosokwani- Longido akielezea namna wakina mama walivyopewa nafasi kubwa katika kumiliki ardhi.
 Dr. Adam Nyaruhume Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro, alieleza kuwa ni muhimu kuwajulisha na kuwaelimisha wanakijiji hasa kuhusiana na maswala ya mipango na matumizi ya ardhi pamoja na umilikishwaji wa ardhi, pia aliwapongeza Asasi ya RUDI kwa kufanya vizuri katika mipango na matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali wanayoyashughulikia.
 Bw. Joseph Rutaizibwa, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi akitoa ushauri kuwa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi kiuchumi lishirikishwe katika michakato hii muhimu inayohusu maswala ya ardhi.
 Bi. Eva Mageni akielezea changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wanawake hasa katika umilikishwaji wa ardhi.
 Bi. Rosada Msoma Afisa Maliasili Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,alisema kuwa Wizara inatoa ushirikiano wa karibu kwa wananchi katika kuhakikisha kuna utunzaji bora wa maliasilizetu.
 Wawakilishi mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi,Wizara ya Kilimo,Wizara ya Mifugo, Wawakilishi wa wakulima na wafugaji, Asasi za Kiraia za Nchini pamoja na za kimataifa,na wadau wengine wakiwa katika makundi mbalimbali kujadili mipango mikakati ya kuendeleza haki za wanawake katika rasilimali ardhi nchini
 Bi. Anne Manangwa Mtafiti kutoka TNRF akitoa mapendekezo kwa niaba ya Asasi za Kiraia ambapo kati ya mambo waliyo omba yafanyiwe kazi katika kampeni  ya wanawake na ardhi ni pamoja na, Elimu itolewe kwa njia ya vyombo vya habari juu ya kumiliki ardhi, haki za wanawake katika kumiliki ardhi pamoja na ushirikishwaji wa wanawake katika kuandaa Sera,uandaaji wa mikakati pamoja na kutunga Sheria.
 Bi. Marcelina Kibena Mwakilishi kutoka MVIWATA, wao katika kikundi chao walitoa maoni kuhusu kutambua makundi mbalimbali kupitia elimu itasaidia kuondoa mfumo dume,kuhamasisha wanawake katika kushika nyadhifa mbalimbali za maamuzi, vyombo vya habari kuandaa programu mbalimbali za uelewa kuhusu kumiliki ardhi na mgawanyo wa rasilimali kuanzia ngazi ya kijiji.
Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Care International,WLAC,PINGOs,UCRT,FFH,LANDESA,PWC,NES
na ILRI pamoja na waendeshaji wa kampeni hiyo Shirika 
la Kimataifa la Oxfam Tanzania pamoja na TALA wakiwa katika warsha hiyo .

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com