Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka Tume
iliyofanya mazungumzo na kampuni ya uchimbaji ya madini Barrick Gold
Mining, kuandaa mazungumzo maalumu ya aina hiyo hiyo kwenye madini ya
Tanzanite na Almasi ili nchi ipate faida na kama wamiliki hao wakikataa
basi waondoke moja kwa moja.
Rais Magufuli amesema hayo leo wakati alipokuwa akipokea taarifa maalum ya mazungumzo kati ya timu ya wataalamu aliyoiunda na timu ya wataalamu kutoka kampuni ya Barrick Gold Mining kuhusu madini ya dhahabu.
"Baada ya tume hii ya dhahabu nataka mfanye 'negotiation' ya namna hii kwenye almasi lakini pia mfanye negotiation kama hii kwenye Tanzanite, Mpangee mapema, muanze haraka. Hakuna kulala. Zege hailali. Lazima tufanye kwa spidi ili Almasi nayo muingie kwenye majadiliano yake tuweze kupata faida. Atakaye kataa kuja kufanya majadiliano atupishe atuache moja kwa moja na madini yetu. Kamati hii imeonyesha njia.... Atakayekataa atupishe. Tutafanya hivyo kwenye madini yote na nyinyi mmeshaonyesha njia," Rais Magufuli .
Pamoja na hayo Rais Magufuli amesema amekubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Prof. Kabudi kuwa iendelee kufuatilia madai yote kwa ajili ya pande zote mbili.
Kwa upande mwingine Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barick nchini imekubali kulipa fidia ya dola milioni 300 ambazo sawa na bilioni 700 za Tanzania, pamoja na kuweka mgao sawa wa faida wa 50/50 na serikali, kufuatia mazungumzo ya ripoti ya makinikia yaliyofanyika kwa zaidi ya miezi mitatu,

0 comments:
Post a Comment