Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa
Maji Profesa Makame Mbarawa ili kuzindua mradi mkubwa wa maji wa
Kibamba-Kisarawe katika sherehe zilizofanyika Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani
leo tarehe 28 Juni 2020.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifungua maji kwenye eneo la mradi wa Kibamba -Kisarawe mkoani Pwani mara
baada ya kuzindua mradi huo mkubwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishika maji ya bomba mara baada
ya kuzindua mradi mkubwa wa Maji wa Kibamba-Kisarawe mkoani Pwani.
RAIS Dkt. John Magufuli amezindua mradi mkubwa wa maji wa
Kibamba-Kisarawe katika Wilaya ya Kisarawe Mkoani wenye thamani ya Tsh. Bilioni
10.6 ambao umekusudia kuondoa tatizo la ukosefu wa maji lililodumu katika
Wilaya hiyo kwa zaidi ya miaka 113 sasa.
Wilaya ya kisarawe sasa inapata maji lita Milioni 6 ukiwa ni mradi wenye dhamani ya
bilioni 10.6 fedha za ndani za Dawasco.
Akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa na Mamlaka ya
Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) leo Jumapili (Juni 28,
2020)kutoka Kibamba hadi Kisarawe, Rais Magufuli alisema kuwepo kwa mradi huo
kumekuwa fursa kwa wakazi wa kisarawe kwa kupata ajira pamoja na maji safi.
“Nilipokuwa nazindua mradi wa maji huko mlandizi iliniumiza
na kunisikitisha kuona wilaya kongwe kama hii katika Tanzania yenye miaka 113
ikae bila maji, ndo maana nikaamulisha maji lazima yafike kisarawe” alisema
Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli alipongeza DAWASA kwa kutanguliza
uzalendo wao mbele katika ukusanyaji wa mapato ya bili za maji, na kufikisha
huduma bora kwa wateja na kusimamia
ipasavyo mradi huo mkubwa wa maji na miradi mingine katika mkoa wa Pwani.
Akifafanua zaidi Rais Magufuli pia aliusifu utendaji kazi wa
watumishi wote wa mkoa wa Pwani kwa hatua kubwa inayopiga kimaendeleo kwa kuendelea kusimamia na kuwa wazalendo katika
miradi usimamizi wa miradi 45 ya maji iyopo mkoani humo, huku akibainisha zaidi
ya Tsh. Bilioni 30.37 zikitolewa mkoani humo kwa ajili ya kugharamia Elimu Bure
katika shule za msingi na sekondari.
Kuhusu huduma za afya, Rais Magufuli alisema Serikali
imeupatia Mkoa wa Pwani jumla ya magari ya wagonjwa 36 kutoka magari 12
yaliyokuwapo hapo awali, huku jumla ya Tsh. Bilioni 12.8 zikiwa zimetolewa
mkoani humo kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na vifaa tiba kwa wananchi.
Akigusia sekta ya Viwanda, Rais Magufuli Mkoa wa Viwanda
unaongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa ya viwanda ambapo hadi sasa, una
viwanda vikubwa 69, viwanda vya kati 88, viwanda vidogo 216 na viwanda vidogo
sana 819 hivyo kuufanya mkoa wa Pwani kuongoza Tanzania kuwa na Viwanda vingi
kuliko Mkoa wowote nchini.
“Unapokuwa na viwanda maana yake ushatengeneza ajira,
unapokuwa na viwanda hata haya maji ya mradi huu utakaokuwa unatoa maji lita
Milioni 6, lakini yanayo hitajika hapa hapa wilayani kisarawe ni lita milioni 1
hivyo viwanda vitasaidia sana hata katika bili
ya kulipa maji” alisema rais Magufuli.
Naye Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa alisema DAWASA
tangu mwezi Juni 2018 ilikuwa inakusanya Bilioni 7.8 kwa mwezi, huku mwezi
machi mwaka huu ikikusanya Tsh. Bilioni 12.5 hivyo kuifanya DAWASA kuwa na
ongezeko la ukusanyaji bili kufikia asilimia 57.6 ya malengo iliyojiwekea.
0 comments:
Post a Comment