Sheikh wa mkoa wa dodoma Mustapha Rajabu akizungumza na wajumbe
wa Baraza la bakwata mkoa kwenye uchaguzi wa mwenyekit na wajumbe wa halimashauri kuu bakwata Mkoa wa Dodoma.
Sheikh wa mkoa wa dodoma Mustapha Rajabu akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza la bakwata mkoa wa Dodoma
japhari Mwenyemba,Mwenyekiti wa uchaguzi huo na Mkurugenzi
wa Elimu Bakwata Taifa,Ally Abdallah pamoja na wajumbe wa baraza la bakwata la mkoa huo.
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Dodoma
limemchagua Japhari Mwanyemba kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza hilo
kwa Mkoa wa Dodoma.
Mwanyemba ambaye amewahi kuwa Meya wa Jiji la Dodoma pia ni
Diwani wa Kata ya Makole Jijini hapa.
Mwenyekiti huyo alichaguliwa juzi Jijini hapa katika
uchaguzi uliowashirikisha wajumbe wa Baraza hilo kwa Mkoa wa Dodoma.
Akitangaza matokeo Mwenyekiti wa uchaguzi huo na Mkurugenzi
wa Elimu Bakwata Taifa,Ally Abdallah alimtangaza Mwanyemba kushinda kwa kura
zote za ndio ambazo ni 37.
Pia,wajumbe hao walimchagua,Kakogwe Luambano kuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Bakwata anaeuwakilisha Mkoa wa Dodoma.
Vilevile waliwachagua Masheikhe 10 ambao ni wajumbe wa
Baraza la Masheikhe Mkoa na Wajumbe 10 wa Halmashauri kuu ya Bakwata Mkoa
wa Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa,Mwenyekiti wa
Halmashauri kuu ya Bakwata Mkoa,Mwanyemba aliomba ushirikiano huku akiwataka
Masheikhe kuyatumia machinjio kama njia ya kuliongezea mapato Baraza.
"Tunajenga Bakwata mpya tunataka kila kitu kionekane na
kinyooke,niwaombe tuliochaguliwa tuwalinde Masheikhe,lakini kubwa tutambue mali
zetu,tukusanye mapato,"alisema.
Kwa upande wake,Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu
aliwataka viongozi hao waliochaguliwa kubadilika, kujitambua na kuacha kuishi
kwa mazoea.
Vilevile,alisema wanatakiwa kuisemea vizuri Serikali ya
awamu ya tano akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi
Wakuu.
"Rais wetu ametuongoza vizuri na maandiko yanasema
waheshimuni na kuwatii wenye Mamlaka,sisi lazima tumtii na kumsemea vizuri Rais
wetu,msemeeni vizuri,"alisema.
Akitoa neno la shukrani,mara baada ya kuchaguliwa,Mjumbe wa
Halmashauri kuu Bakwata anaeuwakilisha Mkoa wa Dodoma,Luambano
alisema,Makatibu,Masheikhe na Wenyeviti wl kuifuata Katiba ya Baraza hilo kwani
kwa kufanya hivyo mambo yataenda vizuri na hakutakuwa na malalamiko.
Naye,Mwakilishi wa Baraza la Masheikhe Mkoa wa
Dodoma,Sheikhe Saidi Rajabu akitoa neno la shukrani aliwataka viongozi wenzake
wa dini kwenda kufanya kazi kwa kumuogopa Mwenyezimungu.
0 comments:
Post a Comment