Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas akiwa na kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim wakiwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MWENYEKITI wa Kamati ya Usalama
Barabarani Salim Abri Asas amewashika mkono majeruhi wa ajali iliyotokea katika
mlima Kitonga wilayani Kilolo mkoani Iringa na aliwaombea uponyaji wa haraka
majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ruafa mkoani hapa.
Asas ameliomba Jeshi la Polisi kumtafuta na kumkamata dereva
huyo aliyekimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo na
majeruhi kwa watanzania ambao walikuwa wamepanda basi hilo.
Alisema kitendo cha dereva huyo kutokomea kusikojulikana
inaaminisha kuwa ajali hiyo ilikuwa ni ya makusudi kwakuwa angekuwepo angetoa
ushirikiano mzuri kwa mamlaka zinazohusika
“Huyu dereva ni muuaji haiwezekani iwe ajali ya bahati mbaya
harafu akimbie badala ya kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi na
usalama ningeomba wenzetu wa polisi wamtafute wamkamate na afikishwe katika
vyombo vya sheria” amesema Salim Asas
Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim ametembelea majeruhi
wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa
baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria Kampuni ya Prezdar
iliyotekea milima ya Kitonga mkoani Iringa
Kamanda Muslim alisema basi hilo lenye naomba za usajili
T326 CSX Kampuni ya Prezdar linalofanya safari zake Iringa – Dar es salaam
liliatumbukia katika maporomoko ya Milima ya Kitonga wilayani Kilolo.
Kamanda Muslim aliwataka madereva kutambua kuwa wamebeba
roho za watu hivyo wanatakiwa kuchukua tahadhari muda wote wanapokuwa
barabarani.
Alisema Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria za
usalama barabarani kwa kuwachukulia hatua madereva wote wanaoendelea kuvunja sharia
za usalama barabarani.
Kamanda Muslim alisema jeshi hilo pia linaendelea kumtafuta
na kumfikisha katika vyombo vya sheria dereva wa basi hilo ambaye alitokomea
kusikojulikana mara tu ilipotokea ajali.
Watu 10 wamepoteza maisha na wengine 36 wamejeruhiwa katika
ajali hiyo huku miili 5 ikiwa tayari imetambuliwa na ndugu zao.
0 comments:
Post a Comment