Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kulia) akizungumza na Mhandisi Mkuu wa
ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Karanga Mhandisi Emmanuel Mwangalaba (SP) alipotembelea
kiwandani hapo kuangalia Maendeleo ya ujenzi.
Baadhi ya vifaa vinavyosubiri
kufungwa katika kiwanda cha Karanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Prof. Riziki Shemdoe akikagua ujenzi unaondelea katika kiwanda cha
kuzalisha bidhaa za ngozi Karanga Mkoa wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe ameitaka kampuni ya Tanelec
- Arusha kuharakisha utengenezaji wa vifaa vya umeme ikiwemo (switch gears ) ambazo zinasubiriwa kufungwa
kwenye kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga kilichopo Mkoani
Kilimanjaro.
Prof. Shmdoe aliyasema hayo alipofanya ziara kwenye kiwanda cha Karanga ambacho
kinajengwa na Shirika la Uzalishaji la Magereza. Lengo la ziara hiyo ni
kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho kipya ambacho kinajengwa
kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni tisa.
Katika ziara hiyo Prof.Shemdoe alikagua ujenzi ambao kwa sehemu kubwa
umekamilika na kinachosubiriwa ni ufungaji wa (switch gears) ambazo
zinatengenezwa na Kampuni ya TANELEC ya Mkoani Arusha.
Prof. Shemode alisisitiza kazi hiyo ifanyike kwa haraka ili wataalamu wa
kufunga vifaa hivyo watakapofika wasiwe na sababu ya kushindwa kujaribu mitambo kwa ajili ya
kukosa umeme.
”Ombi langu
kwa Tanelec mhakikishe mnatengeneza kwa wakati vifaa vya umeme ili
vifungwe na kufanyiwa majaribio ili wataalam wa kufunga mashine wakija kusiwe
na kikwazo”.
Aidha aliwasihi wasimamizi wa ujenzi kuhakikisha wanamalizia kazi
zilizobakia kwa haraka kwenye ujenzi wa majengo ya awamu ya kwanza.
"Nategema baada ya kukamilika kwa majengo haya uzalishaji utaongezeka mara
dufu".
Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi huo Mhandisi Mwangalamba (SP)
alimueleza Katibu Mkuu kuwa ujenzi huo ungekuwa umekamilika ila changamoto yao
ni utengenezaji wa vifaa vya umeme kutoka Kampuni ya Tanelec kuchukua
muda mrefu hivyo baadhi ya vifaa haviwezi kufungwa mpaka hapo (switch
gears) zitakapofungwa.
Ujenzi wa majengo ya kiwanda cha Karanga unatekelezwa na shirika la
Uzalishaji la Magereza tangu Juni, 2019 na unatarajiwa kukamilika mwaka huu.
Kiwanda Cha
Karanga kitakapokamilika kinatarajia kutoa ajira 5000 za moja kwa moja na
zisizokuwa rasmi 4000 kutokana na shughuli mbalimbali katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment