METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 7, 2017

POLEPOLE ASISITIZA WATAKAO TUMIA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA CCM KUADHIBIWA VIKALI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndug Humphrey Polepole leo tarehe 07 Septemba, 2017 amehudhuria katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Wanging'ombe
Mkoani Njombe akimuwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Ndugu Philipo Mangula.

Mkutano Mkuu huo wa Wilaya ukiwa ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali za ndani ya Chama zinazoendelea Nchini kote ulihudhuriwa na jumla ya wajumbe 718 kutoka kata zote Ishirini na moja za Wilaya ya Wanging'ombe.

Katika Mkutano huo Ndg.Polepole aliwapongeza wanachama na Viongozi wote wa Chama Wilaya ya Wanging'ombe kwa kazi kubwa ya Ushindi wa asilimia mia moja katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kushinda viti vyote vya Vitongoji, Vijiji Udiwani, Ubunge, na kura nyingi walizompatia Rais.

Mbali na hilo Ndg Polepole aliwasisitiza wajumbe wa Mkutano Mkuu kuchagua viongozi waadilifu, wachapa kazi, wanaochukizwa na Rushwa, wanaopenda watu zaidi kuliko wanavyojipenda wao na yote kwa yote wanaokisi utendaji kazi wa Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu John Pombe Joseph Magufuli ili kuendana na kasi ya CCM Mpya ambayo ndio  chachu ya Tanzania Mpya.

Ndg. Polepole aliendelea kwa kueleza juu ya kazi moja kubwa ya Chama Cha Mapinduzi kwa kumnukuu Mwl. Nyerere"Kazi kubwa ya Chama Cha siasa ni kuwasemea watu na kua kama daraja kati ya watu na serikali inayowaongoza", Hivyo Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ni lazima muwasemee watu popote mlipo ili hata wasio wanaCCM waone na waendelee kuamini ninyi ni watu sahihi.

Zaidi Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi alieleza juu ya umadhubuti wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) kikiwa ni Chama bora kwa Itikadi,  Muundo, Utendaji, Idadi kubwa ya Wanachama hai mpaka sasa kina jumla ya wanachama wanaokadiriwa Milioni 14,  kwa Afrika kikifuatiwa na ANC cha Afrika ya Kusini na kikishika nafasi ya Pili Duniani kikiongozwa na Cha cha Kikomunisti cha watu wa Uchina. Hivyo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ni lazima mtembee kifua mbele Afrika na Dunia kwa ujumla kua tupo kwenye Chama sahihi na madhubuti chenye kujali Demokrasia kuanzaia ngazi ya Mashina.

Ndg. Polepole alimalizia kwa kueleza dhamira njema ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Ndg. Magufuli katika kupambana na wala rushwa, wahujumu uchumi, mafisadi na akiweka msisitizo kwamba wote watakaobainika kushiriki uchakachuaji wa pembejeo za wakulima CCM imeelekeza Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Uchaguzi wa leo Wilaya ya Wangilombe ni muendelezo wa Chaguzi mbalimbali zinazoendelea Nchi nzima zikianza ngazi ya Mashina na sasa ni Ngazi za Wilaya.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com