Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akionyesha namba
yake ya ushiriki ambayo ni namba 6 mara baada ya kuzungumza mbele ya wajumbe kuwaomba
kura
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitumia haki
yake ya kikatiba ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya CCM
Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi
wakifatilia mkutano huo uliomalizika kwa salama na amani
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa kwa kishindo. katika nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati) akiwa
na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) na Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake leo Ndg Hassan Tati wakifatilia mkutano Mkuu wa CCM
Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa kwa kishindo
Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa
wakifatilia mkutano huo uliomalizika kwa salama na amani.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na wagombea wengine wa nafasi hiyo akionyesha namba
yake ya ushiriki ambayo ni namba 6 mara baada ya kuzungumza mbele ya wajumbe kuwaomba
kura.
Na
Mathias canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu Leo Jumamosi Octoba 7, 2017 amewazidi mbinu za ushawishi
washindani wenzake 10 waliokuwa wakiwania nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.
Wajumbe 989 kati ya wajumbe halali waliojiandikisha 1034
wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wamemuwezesha Mhe Mtaturu kuwa kinara
katika matokeo hayo kwa kuungwa mkono kwa kura nyingi.
Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha
Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa kauli moja wametumia haki yao ya
kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za
Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.
Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Shule ya
Sekondari Ikungi eneo na Kata ya Ikungi
na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya
kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.
Mjumbe huyo wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mhe Mtaturu
ataungana na wenzake walioshika nafasi ya pili na ya tatu ambao ni Mwanga Ally
Juma aliyepata kura 620, na Yunde Celestine Kimu aliyepata kura 612 kuwakilisha
Wilaya ya Ikungi katika kikao muhimu cha maamuzi cha CCM Taifa.
Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara
baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM
Taifa Mhe Mtaturu amesifu imani kubwa aliyoonyeshwa na wajumbe wote huku
akiwasihi kuonyesha zaidi ushirikiano katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na
jumuiya zake.
Aliahidi kutekeleza na kusimamia kwa vitendo ilani
ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 huku akiwasihi wananchi
kwa kauli moja kushirikiana na Viongozi wote wa Chama na serikali hususani
kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia wananchi pasina kujali
maslahi yake binafsi.
Mhe Mtaturu aliwasihi wajumbe wote kuwaunga mkono
washindi wa nafasi zote za uongozi ndani ya CCM ili kuongeza ufanisi na
uwajibikaji katika kuwatumikia.
Aliongeza kuwa katika kipindi cha uchaguzi wa ngazi
ya chama na hata serikali kila mwananchi huwa na maono na mtazamo wake kwa
kiongozi amtakaye lakini pindi anapochaguliwa kiongozi mmoja ni wazi ni vyema
ikawa mwisho wa makundi hayo hivyo kuwa na mshikamano mpya katika uwajibikaji.
Wagombea wengine ambao hawajafanikiwa kuvuka kiunzi katika
nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni pamoja na Ayubu Heleni
Petro, Bollosi Tatu Mohamed, Mghenyi John Mathias, Mghenyi Juma Shabani,
Mkhotya Prorice Patrick, Muna abubakar Omary, Siphy Iddy Selemani, na Sunja
Mussa Ntandu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment