Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii
Bw. Patrick Golwike akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya katika
Kijiji cha Mondo, kilichopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi Mkoani
Mwanza, mapema.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera
na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bw. Atupele Mwambene akisalimiana na akinamana wa Kijiji cha
Mondo, Kata ya Mondo Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza wakati alipofika
kijijini hapo kuhamsha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo yao
kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao.
Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya
Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Mwajina Lipinga(kulia) aliyeshika
chepeo) akishirikiana na wananchi kujenga jengo la Kituo cha Afya cha
Kijiji cha Mondo Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kutatua kero ya
ukosefu wa huduma za afya katika kata ya Mondo kwa kutumia nguvu za
wananchi wenyewe.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera
na Mipango Bw. Atupele Mwambene(kushoto walioshika chepeo) akichanganya
saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha
Mondo, Kata ya Mondo kilichoko Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza katika
kuhamsha ari ya kushiriki kazi za maendeleo kwa kutumia rasilimali
zilizopo katika mazingira husika.
Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya
Jamii Ufundi, Misungwi Mhandisi Harold J. Mtyana akishiriki kujenga
jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mondo, kata ya Mondo, wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii
Bw. Patrick Golwike akikabidhi mifuko 50 ya simenti kwa niaba ya Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mondo Bw. Marthias Lumwagila kwa
ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa Kituo hicho cha Afya.
Sehemu ya jengo la kituo cha Afya
cha Mondo, Kata ya Mondo,Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kama
linavyoonekana na wananchi wakiendelea na kazi ya ujenzi.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Sera ya Maendeleo ya Jamii pamoja
na mambo mengine, inaelekeza jamii kushiriki kazi za kujiletea
maaendeleo yao wenyewe maana jamii ndiyo kitovu cha maendeleo.
Kwa kutambua hilo, Mkurugenzi wa
Maendelo ya Jamii Bw. Patrich Golwike ametembelea katika Kijiji cha
Mondo, Kata ya Mondo, kilichopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza
kuhamsha ari ya wananchi kushiriki katika ujenzi wa jengo la Kituo cha
Afya cha kijiji chao.
Bw. Golwike alibainisha kuwa
maendeleo ya mtu ni mtu mwenyewe na hakuna mtu kutoka nje ya eneo fulani
ataleta maendeleo katika eneo husika.
“Sisi hatukuja hapa kijijini Mondo
kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya Mondo, bali tumekuja
kuhamsha ari ya wananchi wa kijiji hiki kuwa tayari kushiriki kazi za
maendeleo yao kwa kutumia rasilimali zilizopo” alisema Bw. Golwike.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya
Mondo Bi. Aziza Omary alibainisha kuwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya
cha Mondo uliibuliwa kwenye kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ya Mondo,
ndipo iliporidhiwa kujenga kituo hicho ili kupunguza tatizo la vifo vya
mama na mtoto wakati wa kujifungua, na pia kuondokana na kutembea
umbali mrefu kufuata huduma za afya za rufaa zikiwemo za wazazi na
wagonjwa wengine.
Awali wananchi walishiriki kubaini
changamoto, kupanga, kutekeleza na kusimamia mradi wa ujenzi
kuhakikisha kuwa wananchi wanajitolea kuchangia nguvu kazi zao katika
zoezi la ujenzi.
Kazi nyingine zinazofanywa na
wananchi ni kukusanya vifaa vya ujenzi kama vile mawe, kokoto, mchanga,
mafundi, na utoaji uchangiaji wa rasilimali fedha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kijiji cha Mondo Bw. Philipo Suleiman ameipongeza Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuchagua kutembelea
kijiji cha Monde mio ngoni mwa vijiji takribani 900 vilivyopo katika
mkoa wa Mwanza.
Jengo la Kituo cha Afya cha Kata
ya Mondo linakadiriwa kukamilika mwaka 2018 na litagharimu takribani
shilingi 150,460,540/- fedha ambayo itatoka kwa wahisani na wananchi
wenyewe.
0 comments:
Post a Comment