METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 15, 2023

MBUNGE MTATURU AGAWA FUTARI KWA WAUMINI WA KIISLAMU IKUNGI//AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KURIDHIA OMBI LA KULETEWA CHAKULA CHA BEI NAFUU

















Na Mathias Canal, Ikungi- Singida....!

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mkoani Singida Mhe Miraji Mtaturu tarehe 15 Aprili 2023 amegawa futari katika msikiti wa Ighuka, msikiti wa Matongo pamoja na msikiti wa Nuur mjini Ikungi.

Mbunge Mtaturu amegawa chakula hicho ikiwa ni sehemu ya sadaka yake kwa waumini wa kiislamu Wilayani humo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na waumini hao, Mhe Mtaturu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ombi la kuletewa chakula cha bei nafuu katika Wilaya ya Ikungi.

Amesema kuwa katika Wilaya ya Ikungi wananchi waliathiriwa na bei kubwa za mazao hususani bei za mahindi ambazo zilipanda kiasi cha wanachi kushindwa kumudu.

Kupanda kwa bei hizo kulisababishwa na upungufu mkubwa wa chakula katika Wilaya ya Ikungi hali iliyosababisha kupanda kwa bei ya nafaka ambapo serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA iliweka vituo vya kuuza nafaka ambapo bei zilishuka.

Mbunge Mtaturu amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini serikali inayoongozwa na Rais Samia imeongeza juhudi katika kuboresha na kujenga miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule, na miundombinu ya barabara.

Kadhalika, Mhe Mtaturu amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe pamoja na uongozi wa NFRA kwa kusogeza huduma kwa wananchi kwa ajili ya ugawaji wa nafaka.

Mhe Mtaturu amesisitiza umuhimu wa waumini wa dini mbalimbali kuendeleza umoja na mshikamano bila kutotofautiana ili kuimarisha shughuli za maendeleo.


MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com