METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 13, 2017

Benki ya NBC Yazindua Klabu ya Biashara Mkoani Mbeya

01
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika (kushoto), akionyesha nembo mpya ya Klabu ya Biashara ya NBC mara baada ya uzinduzi rasmi wa klabu hiyo mjini Mbeya hivi karibuni. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa waandamizi wa serikali mkoani humo. Wanaoangalia nyuma yake ni Ezekiel Mwakibinga, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Essau Kamwela.
02
Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA), Gabriel Mwangosi (kulia), akifundisha masuala mbalimbali kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati mjini Mbeya. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani Mbeya hivi karibuni.
03
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika (kushoto), akikaribishwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Alvis Ndunguru wakati akiwasili kwa ajili ya uzinduzi wa  Klabu ya Biashara ya NBC mkoani Mbeya. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe. Uzinduzi huo  ulitanguliwa na semina ya siku moja   juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.  
04
Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC, mkoani Mbeya. Uzinduzi huo  ulitanguliwa na semina ya siku moja   juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.  Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa wa serikali mkoani humo.
05
Baadhi ya wateja wa NBC  mkoani Mbeya wakijipiga picha wenyewe ‘maaarufu kama selfie’ wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC mkoani humo hivi karibuni. Uzinduzi huo  ulitanguliwa na semina ya siku moja   juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati  ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa waandamizi wa serikali mkoani humo.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com