Na Masanja Mabula – Pemba
SERIKALI
ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeanza kutekeleza kwa vitendo maagizo
ya Rais wa Zanzibar kwa kugawa majukumu ya utekelezaji wa maagizo
hayo kwa maofisa Wadhamini wa Wizara na taasisi za Serikali Kisiwani
Pemba.
Akizungumza
katika kikao cha kutathmini ziara ya Rais katika Mkoa huo , Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman amewataka wakuu wa Idara za
Serikali kuwa wakweli na wawazi ili kuendana na kasi ya utendaji wa Rais
kwa kuhakikisha maagizo hayo wanayafanyia kazi .
Amesema
kila Wizara inapaswa kushiriki katika kusimamia utekelezaji wa maagizo
hayo yaliyotolewa na Rais wakati wa ziara yake mwezi uliopita katika
Mkoa huo.
“
Ni vyema kila mmoja anatakiwa kuwajibika kusimamia utekelezaji wa
maagizo ya Rais Shein aliyoyatoa wakati wa ziara yake katika Mkoa wetu ,
hii itasaidia kwenda kasi na Rais wetu ”alieleza.
Wakichangia
katika kikao baadhi ya maofisa wadhamini wamesema tayari wameanza
kuyafanyia kazi maagizo ya Rais kwa kufanya ziara na mikutano ya
watendaji wa taasisi zao.
Mapema
Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Ahmed Khalid Abdalla amewapongeza
maofisa wadhamini kutokana na mchango wao uliofanikisha ziara ya Rais
katika mkoa huo .
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid amewasisitiza wakuu hao wa
taasisi kuhakikisha wanawajibika katika kutekeleza maagizo ya Rais kwa
uwazi ili wananchi wazidishe imani na serikali yao.
0 comments:
Post a Comment