MENEJA wa mfuko wa taifa wa bima
ya afya (NHIF) mkoani Pwani ,Fortunata Raymond ,akionekana kuzungumza
jambo katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani hapo
yaliyoandaliwa na mfuko huo
Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani
,Zuberi Samataba wa kwanza kulia ,akizungumza katika mafunzo ya siku
moja kwa waandishi wa habari mkoani hapo yaliyoandaliwa na NHIF Mkoa wa
Pwani, wa kwanza kushoto ni Meneja wa mfuko huo mkoani humo Fortunata
Raymond
Baadhi ya waandishi wa habari
mkoani Pwani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi kutoka mfuko
wa taifa wa bima ya afya mkoani humo .Picha na Mwamvua Mwinyi
……………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WAANDISHI wa
habari ,hasa wasio na mikataba maalum katika vyombo vyao mbalimbali vya
habari ,wametakiwa kujiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya afya ili
kujihakikishia usalama wa afya zao wawapo kazini .
Aidha
endapo wakitumia kalamu zao kuelimisha makundi ya wajasiriamali
,wanafunzi wa vyuo ,watoto chini ya miaka 18,wafanyakazi
viwandani,viongozi wa dini ,umuhimu wa kujiunga na bima ya afya
itaongeza wigo wa watu kujiunga na huduma hiyo.
Rai
hiyo ,imetolewa na katibu tawala wa mkoa wa Pwani ,Zuberi Samataba
,wakati akifungua warsha fupi kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na
NHIF mkoani hapo .
Alisema tasnia hiyo inakumbana na hatari na kufanya kazi katika mazingira magumu ambayo yanahitaji kuwa na Bima .
Alisema tasnia hiyo inakumbana na hatari na kufanya kazi katika mazingira magumu ambayo yanahitaji kuwa na Bima .
Samataba alieleza ,wapo
waandishi wa habari ambao ni vinara wa kuandika makala na kuelimisha
kuhusu NHIF na CHF lakini wao wenyewe hawajajiunga .
Alibainisha ,mafunzo
hayo yawe chachu cha mabadiliko kwao kuona Bima ya afya ni sehemu ya
vitu muhimu katika maisha na kazi zao .
“Majukumu yenu
yamezungukwa na mazingira magumu na hatarishi hivyo ni muhimu mjiunge na
mfuko wa taifa wa bima ya afya ili kuwa na uhakika wa kutibiwa mahala
popote pindi mnapopata tatizo”alisema Samataba.
Hata hivyo Samataba ,alieleza kutokana
na mkoa wa Pwani kuendelea kutoa fursa nyingi za ajira kupitia sekta ya
viwanda ni vema wafanyakazi hao wakajiunga na mfuko huo.
“Watumishi
wa sekta binafsi nao wana fursa ya kujiunga ,inasaidia kuwa na uhakika
wa kugharimia matibabu pale wanapoumwa na hata kama hawana fedha za
matibabu ,” alisema .
Aliwahakikishia ,
serikali inazidi kuuboresha mfuko wa taifa wa bima ya afya ili wanachama
wake wanapokwenda kutibiwa katika zahanati na vituo vya afya
wasisumbuliwe wala kukosa dawa.
Samataba alisema kwa
sasa serikali inafikiria kuwa na huduma ya afya kwa wote ambao kila
mwananchi atalazimika kujiunga na huduma hizo.
Nae
meneja wa mfuko wa taifa bima ya afya mkoa wa Pwani,Fortunata Raymond
,alisema warsha hiyo itawajengea uwezo waandishi wa habari hao kujua
faida na manufaa ya bima za afya.
Alisema, wameanza utaratibu wa kuwaunganisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kupitia mpango wa TOTO KADI.
Fortunata alielezea ,mpango huo ni wa gharama nafuu kiasi cha sh.50,400 pekee na mtoto huyo ataweza kupata huduma kokote nchini.
Pamoja
na hayo ,alibainisha kwamba, sekta isiyo rasmi ikiwemo vibindo, saccos,
amcos, vikoba na vikundi maalumu vya wajasiriamali vilivyosajiliwa nayo
itanufaika .
“Utaratibu
wa vikundi hivi unaitwa VIKOA ambapo vikundi vyenye mwelekeo wa
kiuchumi vitapata fursa ya kujiunga ,hawatatumia fedha za mitaji yao kwa
ajili ya kujitibia “alieleza Fortunata.
Fortunata alisema , mfuko huo zamani ulikuwa ukitoa huduma kwa
watumishi wa serikali pekee lakini sasa wanategemea maboresho makubwa
ili kufikia watanzania wengi.
Alisema
wanatarajia kuongeza elimu kwa wadau ,kuboresha kitita cha
mafao,usambazaji na utoaji huduma vijijini,kuimarisha usajili wa maduka
ya dawa muhimu na utoaji wa vitambulisho vipya kwa wanachama.
Meneja
huyo wa NHIF mkoani humo,alifafanua tangu waanze kutoa huduma hizo
ndani ya jamii ni miaka 15 sasa na tayari kuna mafanikio makubwa hapa
nchini.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la habari leo mkoani Pwani,John Gagarini ,alisema
waandishi ambao hawana ajira za kudumu wamekuwa wakishindwa kujiunga
tofauti na wale walioajiriwa wanaonufaika kwenye mikataba yao moja kwa
moja.
Alisema
utaratibu mpya wa VIKOA utawezesha waandishi ambao hawajajiunga na
huduma hizo kujiunga kupitia vyama vyao vya mikoa kwa gharama y
ash.76,800 kwa kila mwanachama.
0 comments:
Post a Comment