METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 12, 2019

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ARINSA NA MKUTANO MKUU WA MWAKA

Baadhi ya Bendera za Nchi wanachama wa ARINSA (Asset Recovery Inter-Agency for Southern Africa), ( , 1-Uganda, 2-Tanzania, 3-Lethoto) zikipitishwa kwa washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu ARINSA, uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , Chama hicho pia kilikuwa kinaadhimisho Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili kufungua Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu, ARINSA uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009, Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine Mahiga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009,kutoka kulia ni Mkuu wa Mpango wa Kuzuia Utakatishaji Fedha, Michiel Van Dyk, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine Mahiga, Kushoto ni Jaji Dkt.Eliezer Mbuki Feleshi, na Mshauri wa UNOC, Fitz Ray Drayton.
Washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu ARINSA, uliofanyika wakifuatilia Mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
*************************
Kutokana na changamoto ya upungufu wa fedha za kuendesha taasisi ya ARINSA kuna ulazimu katika mali zilizotahifishwa kuwepo kwa mgawanyo wa asili,ia kadhaa ziende kwa ofisi zinazoendesha mashtaka  na nyingine ziende kwa taasisi ya ARINSA.
Ameyasema hayo leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika maadhimisho ya miaka 10 ya ARINSA na mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Nafahamu kuwa umoja huu umetanua wigo wa ushirikiano katika masuala ya upepelezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kiupelelezi zinazosaidia kuharakisha kukamilika kwa maombi ya ushahidi nje ya nchi na upatikanaji wa mali zinazohusiana na uhalifu”. Amesema Mh. Samia.
Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa ni heshima kubwa kwa nchi yetu kuwa ni mmoja wa nchi ambazo zipo katika umoja wa ushirikiano wa kudhibiti uhalifu nchini na Afrika kwa ujumla.
Pamoja na hayo Rais wa ARINSA Bw. Biswalo Mganga amesema kuwa wanataka kuhakikisha wote ambao wanajihusisha na uvunjifu wa amani wanashughulikiwa ili kuwemo na amani katika wanachama nchi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com