*****************************
Serikali imekua na mikakati mikubwa ambayo imesaidia kuwatoa Watoto
katika suala zima la utumikishwaji katika kazi na mazingira mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Bungeni kuhusu maadhimisho ya siku ya kupiga vita utumikishwaji dhidi ya
Watoto.
Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Dkt. John Pombe Magufuli imekua ikichukua hatua mbalimbali dhidi ya
tatizo hilo.
“Jamii inatakiwa kutambua maana ya utumikishwaji wa Watoto na kazi
hatarishi zinazowakabili ili kuwa walinzi wa watoto,” alisisitiza Mhagama.
Aliongeza kuwa Watoto hawatakiwi kutumikishwa bali wasaidiwe kutimiza
ndoto zao kwa kuwaandaa kuwa raia wema na wajenzi wa Taifa la kesho.
Alieleza juu ya Sheria na mikakati mbalimbali inayosimamia haki za Watoto
ikiwemo Sheria ya elimu ambayo inataka Watoto wote kupata fursa ya
elimu, Sheria Na. 1 (2009) ambayo inalinda haki na ustawi wa mtoto,
Sheria Na. 6 (2004) ya Ajira na Mahusiano Kazini inelezea mazingira
ambayo mtoto hatakiwi kutumikishwa kazi ambazo hazipo kwa mujibu wa
taratibu.
Pamoja na hilo alielezea pia juu ya mpango ya taifa wa kupiga vita ukatili
dhidi ya Wanawake na Watoto ambao umesaidia katika kuwaondoa Watoto
kwenye mazingira hatarishi na Mpango Mkakati wa taifa wa kupambana na
ajira dhidi ya Watoto.
“Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia viwango vya kazi na imekuwa ikisisitiza
waajiri kufuata sheria za kazi kwa kutowahusisha Watoto katika
mazingingira hatarishi au kwenye kazi zisizo na staha ambazo zinafanya
Watoto waingie kwenye utumikishwaji,” alisema Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa jamii kuwapa Watoto kazi
zinazozingatia umri, ukubwa wa kazi na zinazolinda afya yao.
0 comments:
Post a Comment