METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 25, 2017

Mume Ajinyonga Baada ya Kumpiga hadi Kumuua Mkewe Akimtuhumu Kuchepuka Nje ya Ndoa

Mkazi wa Misungwi, Kwilokeja Boniface (35) amemuua mkewe Shija Luchagula (30), kwa kumnyonga kisha na yeye kujinyonga kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana  Jumatatu kuwa tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha Mwiligiligili wilayani Misungwi.

Alisema mwanaume alitoka shambani akakuta tairi nyingi za baiskeli kwenye uwanja wa nyumba yake ndipo ukazuka ugomvi baina yao akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao hivyo alianza kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga mpaka akafariki dunia.

Alisema baada ya kufanya hivyo na yeye alichukua jukumu la kujinyonga kwa kamba ili kukwepa mkono wa sheria.

“Kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na vifo hivyo na miili ya marehemu tayari imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi"
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com