Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ,Gilles Muroto,akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kutokana matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,akionesha mabasi yaliyokamatwa yakiwa yanasafirisha mafuta aina ya Petrol na Disel lita 2127 kwa njia hatarishi kwenda sehemu mbalimbali za mkoa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,akionesha Pikipiki zilizokamatwa zilizokuwa zikitumika katika uporaji.
…………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea na msako mkali huku likiwashikilia watuhumiwa 72 na mabasi matano ya abiria  yaliyokuwa yakisafirisha mafuta aina ya Petrol na Disel lita 2127 kwa njia hatarishi kwenda sehemu mbalimbali za mkoa huo.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ,Gilles Muroto amesema kuwa mabasi hayo yalikuwa yakisafirisha mafuta hayo na abiria ndani yake jambo linalohatarisha usalama wao.
“Tumekamata lita 1277 za Petrol, 850 za Disel na watuhumiwa tisa wakisafirisha kwenye mabasi ya abiria na abilia wakiwemo ndani jambo linalo hatarisha Maisha, kama mtakumbuka tumepoteza watu wengi kwa ajali zinazosababishwa na mafuta.”amesisitiza Muroto
Aidha amesema kuwa  Gari ya kwanza ilikuwa ni Scania Bus T.509 ACV kampuni ya mshikamano lilikuwa limebeba Petrol lita 137 na Disel lita 20,Toyota Costa T.493 DPA lilibeba mafuta lita 40, Toyota Hiace T. 637 DNY  abilia na Petrol lita 140, TATA T.637 DGN Petrol lita 390 na Disel lita 360, Scania Bus T.783 ASY Petrol lita 580 na Disel lita 380”Alisema Muroto
Kamanda Muroto amefafanua kuwa Katika msako huo walimkamata Jonathan Temu (41)  akiwa na nyama ya wanyama Poli NSYA wanne na DigiDigi mmoja  wenye thamani ya 2,87500 alio wapata kwa uwindaji haramu
Hata hivyo amesema kuwa  wanaendelea na msako wa kukomesha uhalifu wamemshikilia kijana mmjo kwa kufanya ujambazi na mabinti wa tatu kwa kufanya biashara ya ukahaba
“Tulimkamata Hosea Mrema(22) boda boda akiwa na kifa cha kuvunjia , na Tumaini Shayo(32) na wenzake wawili wakifanya ukahaba maeneo ya uhindini kata ya viwandani” amesema Muroto
Kamanda Muroto amesisitiza kuwa operesheni iliendelea na walikamata Mirungi, Bhangi na Pombe ya Moshi na mitungi miwili ya kutengenezea gongo katika maeneo tofauti tofauti ya jiji
Hata hivyo amesema kuwa Kijana Musa Tengu(30) na wenzake wawili tuliwakamata wakiwa na robo kilo ya mirungi, Rashid Rashid(42) na wenzake saba walikamatwa wakiwa na pombe halamu lita mbili, na Sophia Paulo na wenzake wawili walikamatwa wakiwa na bhangi gram tisa.
Kwenye msako huo wamemkata John Daniel(24) boda boda mkazi wa Ihumwa akiwa na piki piki isiyo kuwa na namba za usajili aina ya boxer mali inayodhaniwa kuwa ya wizi
“Watuhumiwa tisa wamekatwa  kwa makosa ya unyang`anyi na kutumia nguvu na tumekamata pikipiki nne watuhumiwa tunawaandalia mashitaka na tutawafikisha mahakamani”Alisema Muroto
Kamanda Muroto amesema kuwa wanaomba  wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani humo ili kuweza kukomesha ama kutokomeza kabisa vitendo vyote vinavyoonyesha kuvunja amani katika nchi yetu